KISUKARI; Kisukari cha mimba ni ugonjwa unaokua kwa kasi SANA
Ugonjwa huu unatajwa kuwapata wanawake wakati wa ujauzito, pasipo wao wenyewe kujua na matokeo yake hujifungua watoto wenye uzito mkubwa, walio na matatizo ya kimaumbile na wengine huzaliwa wakiwa na rangi ya manjano.
Ugonjwa huu unatajwa kuwapata wanawake wakati wa ujauzito, pasipo wao wenyewe kujua na matokeo yake hujifungua watoto wenye uzito mkubwa, walio na matatizo ya kimaumbile na wengine huzaliwa wakiwa na rangi ya manjano.
Wataalamu wanaeleza kuwa ugonjwa huo unashika kasi duniani na kwamba wanawake wajawazito, ambao huongezeka uzito kwa kasi katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wao, wanakabiliwa na hatari zaidi ya kupata kisukari cha mimba.
Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumamosi, Mkuu wa Idara ya Kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kisukari, Dk Mohammed J Mohammed anasema kuwa ugonjwa huo huwapata kinamama hao hasa kipindi cha miezi sita au zaidi ya ujauzito.
Kisukari cha mimba humpata mwanamke kipindi cha ujauzito hasa katika kipindi cha mwisho kuanzia wiki ya 24 na kuendelea. Kisukari hiki hakidumu kwa muda mrefu kwani kinaweza kupotea mara tu baada ya mama kujifungua, lakini pia kinaweza kuendelea na hapo tunasema kimebadilika kuelekea katika hatua nyingine,” anasema Dk Mohammed.
Anasema kuwa idadi kubwa ya wanawake hawafanyi vipimo vya kisukari cha mimba wanaokuwa wajawazito mijini na vijijini hivyo kutojua hali zao kiafya na kama wapo katika hatari ya kupata kisukari cha mimba.
idadi kubwa ya wanawake hawafanyi vipimo, hawa hujifungua bila kujua wana tattizo hilo hatima yake linaisha. Lakini wapo pia ambao huendelea na tatizo hilo na baadaye linakuwa kubwa.”