Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anaelezea kuwa kwenye mashine maalumu kunakuwa na mipira kadhaa ikiwamo ya kupitishia damu kupeleka kwenye figo bandia, inayofanya kazi kama ya mwilini na mirija mingine ambayo ni mikubwa kiasi inatumika kutoa maji yasiyohitajika mwilini na sumu, huku mingine ikitumika kurudisha damu safi mwilini.
 
Mgonjwa hulala akifanyiwa tiba hii kwa saa nne, bila kuchomwa sindano ya usingizi, kwa kuwa haina maumivu makali. Vilevile mgonjwa hutobolewa eneo maalumu mwilini kwa ajili ya kupitishia mipira. Kuna wanaotobolewa shingoni au mkononi kulingana na anavyotaka mgonjwa," anasema Dk Kisanga.
 
Anaendelea kuwa kazi nyingine za figo ni pamoja na kusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoletin ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, pia kusaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…