Njia tano bomba kwa afya yako
1. Apple moja kwa siku - hukuweka mbali na daktari.
2. Jani la mrihani (tulsi leaf) ukitumia kwa siku hukuweka mbali na saratani
3. Limao kwa siku -hukuweka mbali na unene
4. Kikombe cha maziwa kwa siku -hakuna tatizo la mifupa
5. Lita tatu za maji kwa siku- hakuna magonjwa.
Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida.
Vyoo vina matumizi mengi ingawa bado watu wengi hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Tanzania wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa.
Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’.
Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa kuwa mkao huo unaweza kuleta matokeo mbalimbali ndani ya mwili.
Utafiti uliofanywa na mtandao wa ‘naturesplatform’ umegundua kuwa matumizi ya choo cha kukaa huweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo kansa ya utumbo mkubwa.
Samwel Shita anasema, madhara ya vyoo vya kukaa ni makubwa kwani wakati mwingine yanaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa kutokana na haja kubwa kubaki kwa muda mrefu katika utumbo huo.
Unapokaa unakuwa umekaa katika choo mwili unakuwa umelegea, hivyo inabidi utumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tofauti na unapochuchumaa,” anasema Shita na kuongeza:
Matatizo huanza hapo, unapojisaidia ukiwa umekaa na kulazimisha kujikamua unaweza kusababisha vimishipa vidogo katika utumbo mpana sehemu ya haja kubwa ya ndani na ya nje kuvimba na maumivu makali husababishwa na ugonjwa unaojulikana kama ‘hemorrhoid,” anasema.
Anasema ‘hemorrhoid’ ni ugonjwa ambao pia huitwa bawasiri. Mgonjwa hupata uvimbe katika njia ya haja kubwa na hivyo kupata maumivu wakati wa kujisaidia na haja yake mara nyingine huambatana na damu.
Kila binadamu anapaswa kujisaidia na kuhakikisha haja yote imetoka na kwisha kabisa, inapobakia inaweza kusababisha maambukizi katika utumbo mpana kwa kuwa ule ni uchafu wenye mchanganyiko wa vitu vingi,” anasema Shita.
Haja kubwa inapokuwa tayari imeshajitengeneza inapaswa kutoka yote, kama itabaki kipindi kirefu inaweza pia kuleta uambukizi katika utumbo mkubwa na hata katika kidole tumbo,” anasema Shita.
Uchafu huu si tu unaweza kusababisha maambukizi, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa. Wote tunajua kuwa mkusanyiko wa sumu mbalimbali mwilini unakuweka katika hatari ya kupata saratani, hivyo tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi mapema linaweza kufikia huku,” anasema Shita.
Daktari Berko Sikirov kutoka Misri ambaye alifanyia utafiti matumizi ya vyoo vya kukaa anasema kuwa iwapo mtu ana tatizo la vivimbe vya ‘hemorrhoid’ linaweza kumalizika iwapo ataacha kutumia vyoo vya kukaa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.