Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sikuangalia nitachekwa kwa umri nilionao kuvaa sare na kwenda chuo kutimiza maono yangu, huko nilisoma darasa moja na wanafunzi wenzangu ambao umri wao ni sawa na wanangu, sikujisikia vibaya nilijitahidi kuwa makini na masomo yangu hatimaye nikahitimu kwa kufaulu vizuri,” anasema.
 
Anasema baada ya kuhitimu kwa kuwa wana eneo kubwa na mume wake aitwaye Michael Mwaipyana walijenga madarasa mawili kisha wakaanza kufundisha watoto huku wakiendelea na taratibu za usajili.
 
Kituo hiki nimekianzisha tangu mwaka 2012 kuna siku walikuja madiwani hapa kunitembelea hapa, wakaridhika na hali waliyoikuta ikiwamo ukubwa wa eneo langu, hivyo wakanishauri niende kwenye ofisi husika ili nisajili,” anasema.
 
Anaeleza alianza kuufanyia kazi ushauri huo mzuri , lakini alishtuka siku moja kiongozi mmoja wa kata akiwa ameongozana na mtu mwingine walifika na kumtaka awape rushwa ya Sh2.5 milioni ili apate huo usajili.
 
Kapange anasema pia baada ya kufuatilia ameona utaratibu na masharti ya usajili ikiwamo la kutakiwa kuwa na akiba ya Sh68 milioni kwenye akaunti yake, jambo ambalo kwake analiona ni gumu kulitimiza.
 
Sharti hili ni gumu binafsi naliona kama linaweza kushawishi mtu kufanya udanganyifu wa kuweka fedha zionekane zipo kwa muda baadaye hali ya akaunti inakuwa ya kiwango kidogo,” anasema.
 
93acc4ba11cec6f8ea5272e20d36d33b.jpg
 
Back
Top Bottom