Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja Rasilimali watu wa TBL, George Albano alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kilichopo Lyunga jijini Mbeya na kujifunza hatua mbalimbali za utengenezaji wa bia.
 
Alitaja madhara ya kimaumbile yanayoweza kumkuta mtoto ni kutokua vizuri, matatizo ya figo, moyo ambapo pia inaweza kusababisha matatizo ya kitabia ikiwemo ufahamu mdogo na maradhi yanayosababisha mtoto kukosa umakini.
 
Alisema baada ya kutambua athari hizo, TBL imekusudia kutoa mafunzo kwa wamiliki, wahudumu wa baa na maduka ya kuuzia pombe na kwamba wanaamini wakipata elimu hiyo watakataa kuwauzia pombe wajawazito na watoto.
 
Aidha, Albano alisema wapo baadhi ya madaktari ambao wamekuwa wakishauri wajawazito kunywa kiasi kidogo cha pombe, Hata hivyo alisema kitaalamu haijathibitika kiwango cha pombe kinachofaa kwa mjamzito na kwamba wanachowashauri ni kwamba wasitumie kabisa.
 
Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu, mtu anapokunywa pombe humfikia mtoto kupitia kondo la nyuma na pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto huathiri uwezo wake wa kupata chakula, virutubisho na hewa ya oksijeni ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine.
 
Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosa usingizi usiku hasa hasa kipindi ambapo mwezi unakuwa kamilifu (full moon), sasa utafiti mpya umepata uthibitisho kwamba mwezi unapokuwa karibu sana na sayari ya Galaxy huwa unatoa athari kwenye usingizi wa binadamu.
 
Christian Cajochen, mtafiti wa masuala ya usingizi kutoka Hospitali ya magonjwa ya Akili ya Chuo kikuu cha Basel, Switzerland, aliongoza utafiti wa kuchambua taarifa za vipimo vya usingizi (ikiwemo utendaji kazi wa ubongo) kwa watu 33 ambao walikuwa wakifanyiwa tathimini kwenye kliniki ya matatizo ya ukosefu wa usingizi usiku.
 
Cajochen alisema “katika kipindi cha mwezi kamilifu (full moon), watu huwa wanapata usingizi mnono (deep sleep) kwa muda mfupi wa kama asilimia 30 ya usingizi mnono wa kawaida, kwa ujumla huwa wanatumia dakika tano kupata usingizi na wakipata usingizi mnono huwa haudumu zaidi ya dakika 20”.
 
miili yetu imekalili tabia za wakati wa usiku (giza) ikiwemo kulala, hivyo ifikapo usiku (giza) miili hutoa vichocheo vinavyotuandaa kulala (sleep-preparatory hormone), vichocheo hivyo kwa kitaalamu hujulikana kama Melatonini hormone. Vichocheo hivi huwa vinapungua sana kipindi cha mwezi kamilifu (kutokana na kuongezeka kwa mwanga wakati wa usiku) na kupelekea mtu kukosa usingizi”. Cajochen alisema.
 
Maelfu ya wanafunzi wako hatarini kupata saratani za vinywa (Oral cancers) kutokana na kuongezeka kwa matumizi holela ya Ugoro (Snuff), Ongezeko la matumizi ya ugoro linakuja baada ya Wizara ya afya na ustawi wa jamii kupiga marufuku uuzaji wa Kuberi.
 
Akiongea na Daily news, mkuu wa kitengo cha afya ya akili na madawa ya kulevya wizarani, Dk norman Sabuni alisema kwamba kutokana na uchunguzi walioufanywa ulibaini kwamba matumizi ya ugoro yameongezeka na wasambazaji wakuu wakiwa ni walinzi wa Kimasai.
 
Alisema kwamba “tunajua idadi ya shule ambazo zimawafukuza walinzi wa kimasai baada ya kugundua kwamba wamekuwa wakiuza Tumbaku kwa wanafunzi. Tumbaku ni halali nchini hivyo tunachokifanya ni mwendelezo wa kuwaonya watu juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku”
 
Alisema kwamba “tunajua idadi ya shule ambazo zimawafukuza walinzi wa kimasai baada ya kugundua kwamba wamekuwa wakiuza Tumbaku kwa wanafunzi. Tumbaku ni halali nchini hivyo tunachokifanya ni mwendelezo wa kuwaonya watu juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku”
 
Back
Top Bottom