Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Afya ya mwili kwa binaadamu ina maana, kuwa na mwili wenye afya usiokuwa na maradhi, afya ambayo kwa kawaida hutokana na kuupa mwili mazoezi ya mara kwa mara, lishe bora na mapumziko ya kutosha. Katika nchi au maeneo ambayo watu wanapata lishe bora, huduma nzuri za afya na kuishi katika hali ya kimaisha inayoambatana na viwango vinavyotakiwa, kwa kawaida vimo na uzito wao huongezeka.
 
Ukweli ni kuwa, ukiwauliza watu wengi afya ni nini, watasema kwamba inahusiana na mwili kuwa salama bila ya kuathirika na ugonjwa. Lakini tukienda ndani zaidi, kitiba afya ya mwili inaamanisha ustawi wa mwili hali ambayo mtu anaipata kwa kutekeleza vipengee vyote vinavyohusiana na afya katika maisha yake.
 
Uzima wa mwili unaakisi kufanya kazi vizuri moyo na mfumo wa kupumua, uwezo wa misuli, viungo pamoja na mwili kuweza kukubali mabadiliko tofauti na muundo wa mwili kwa ujumla. Masuala mengine ni pamoja na lishe bora, uzito wa mwili, kutokuwepo uraibu wa madawa ya kulevya, pombe, mahusiano salama ya kimwili, usafi kwa ujumla na pia kulala na kuamka kwa wakati unaotakiwa.
 
Afya ya akili au uzima wa kiakili ni utambuzi wa mtu na uzima wake kisaikolojia. Mtu ambaye ana afya nzuri ya kiakili hana matatizo ya kiakili au kichaa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, 'afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahamili mfadhaiko (stress) unaotakana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha. Aweze kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.'
 
Ni rahisi watu kuelezea maana ya ugonjwa wa akili kuliko afya ya akili. Watu wengi wanakubali kwamba afya ya akili ni kutokuwepo ugonjwa wa akili lakini maana hiyo haitoshi. Hii ni kwa sababu kama tutachagua watu 100 ambao hawana kichaa au ugonjwa wa akili unaoweza kutambuliwa na daktari wa akili, lakini miongoni mwao tunaweza kuona kwamba afya ya baadhi yao kiakili imeimarika kuliko wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…