Tafiti zinaonesha kuwa maambukizi kwenye kinywa huweza kuwa na uhusiano na magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari, n.k ambayo ni ya kawaida miongoni mwa wazee. Ukweli ni kwamba inakuchukua hatua chache tu kupiga mswaki na kufanya flosi , kumtembelea daktari wa kinywa na meno pamoja na kula mlo kamili ili kuwa na afya safi ya kinywa maishani.