Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ZANZIBAR ni visiwa vya kipekee na upekee huo umepelekea vipewe majina mbali mbali na miongoni mwa hayo ni visiwa cha Viungo (The spice islands). Jina hilo limechangiwa na kuwa kwake na utajiri mkubwa wa viungo ambavyo hupatikana takriban katika mzunguko wote wa misimu ya mwaka.
 
Wazanzibari wenyewe wanalifahamu hilo.na katika jitihada za kuhakikisha wanavifaidi vyema viungo hivyo wamekuwa wabunifu wa mbinu mbali mbali za kuvisarifu na kuvitumia kwa mafanikio zaidi au kwa muda mrefu. Moja ya mbinu maarufu ya kuvisarifu viungo inayotumiwa hapa Zanzibar ni ya Utengenezaji wa Achari.
 
Kwa sababu Zanzibar ni visiwa vya watu mchanganyiko na utamaduni mchanganyiko siajabu sana kwa Achari yenye asili ya Uhindini kutumika hapa Zanzibar. pengine wakati ilipoaanza kungia hapa watengenezaji na watumiaji walikuwa Wahindi pekee napengine wenzao wenye asili ya Asia.
 
Bibi Saada Omar Rajabu alinisimulia na kusema yeye alijifunza upishi huu wa kutengenza achari kutoka kwa Muhindi ,wakati huo yeye bi Saada akiwa ni mtoo mdogo mwenye umri wa miaka 10 . “Nakumbuka nlikuwa sijapelekwa hata chuoni” alisema bi Sada.
 
Anasema ilikuwa bahati tu kwamba alipata wasaa wa kujifunza shughuli hizo kabla ya kuolewa kwani siku hizo wasichana walikuwa wanaolewa wadogo sana. “Namshukuru marehemu mama yangu ndiye aliyekuwa ananipa moyo wa kujiendeleza katika harakati za kiuchumi na kuibuwa mambo mbali mbali badala ya kukimbilia kuolewa” aliongea.
 
Achari ya Embe
Achari ya embe haina kazi sana ya kutengenza isipokuwa ni tabu kuyapata maembe mpaka siku za msimu hadi msimu,zamani watu wengi hawana taaluma ya kufanya achari kama hizi ni watu wachache waliyokum\wa na taaluma kama hii.Alisema bi saada
 
Mahitaji

Achari hii una chukuwa embe zako na kuzitia kwenye chombo chako kikubwa pamoja na maji , kisu, kibati cha kuchunia , unatayarisha chupa yako, unamenya, embe zako, baadae ukishamaliza unazichuna kwenye chombo chengine ambacho ni kisafi
 
Ukimaliza kuchuna unaitia kwenye chupa yako, unaitia chumvi kiasi , pilipili, kiasi,kitungu maji kidogo ili kudhidi kuongeza ladha nzur na kutokea harufu nzur achari yako, kuimaliza hapo una subiria kidogo tu, kwa muda wa dakika {5} mpaka iweze kuchanganyika kwa vitu hivyo na hapo sasa tayar kwa kuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…