Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuangalia sinema za bure mtandaoni ni njia rahisi hasa unapotaka kuangalia sinema zile unazozipenda ukiwa nyumbani kwako, vifaa unavyoweza kuvitumia wakati wa kuangalia sinema hizo ni kompyuta au televisheni iliyounganishwa na mtandao.
 
Kuna maeneo mengi ya kuangalia sinema za mtandaoni, lakini yaliyoorodheshwa katika makala haya yana sinema nyingi, ni salama kwa kompyuta yako na ni halali kwa kutumia, lakini pia kuna programu mbalimbali zitakazokufanya ufurahie huduma zao hata kupitia mawasiliano yako ya mkononi yaani simu.
 
Hizi si sinema fupi bali ni ndefu utakazoweza kuziangalia kupitia mitandao mwanzo mwisho. Sinema mbalimbali zinaweza kupatikana huko ikiwemo za vichekesho, maigizo, zile za zamani, zilizotengenezwa kupitia studio kubwa duniani.
 
Crackle. Kupitia ushirikiano wao na Sony, picha zao zina ubora wa hali ya juu na zenye urefu kamili ambapo unaweza kuzitazama zikiwa na viwango katika sauti na hata picha mjongeo, ni sinema kutoka kwa nyota wakubwa unaowajua pia zinaweza kufunguka kupitia kioo chochote ulichoamua kutumia kuangalia hata kiwe chenye ukubwa wa kiasi gani.
 
Popcornflix. Ni sehemu nyingine nzuri ya kuangalia sinema za mtandaoni. Mtiririko wao wa mara kwa mara wa filamu mpya utakuwezesha kujua ingizo jipya la filamu duniani na kuitazama kwa wakati. Hii ina sinema zaidi ya 1,500 zinazojumuisha vichekesho, matamasha, sinema za kifamilia za mahakamani na za kigeni.
 
Viewster Logo. Huko kuna mkusanyiko wa sinema za bure mtandaoni, Mbali na sinema hizo kuna maonyesho kadhaa ya televisheni unayapakua bure. Ni mkusanyiko wa filamu ambazo hujazisikia zilizotengenezwa kutoka tamaduni tofauti lakini zilizoambatana na matangazo.
 
Nunua mswaki mpya kila baada ya miezi mitatu mpaka minne
Mswaki unakata miaka hata mitatu aisee. Meno siyo kipaumbele cha wengi mpaka yakilianzisha ndo tunayakumbuka. Wanasayansi sasa wanatuambia kwamba afya ya meno inafungamana moja kwa moja na afya ya moyo; na maambukizi yanayoanzia kwenye meno yanaweza kumalizikia kwenye moyo na kuleta madhara makubwa. Tuyajali meno yetu!!!
 
Yidio. Hii ni jamii ya mtandao ulioundwa kwa ajili ya kuonyesha sinema mitandaoni. Ni rahisi kutizama sinema za bure kwenye Yidio, lakini kubwa zaidi ni kusheheni ya miziki, sinema, picha za wanyama na filamu za magharibi.
 
Wengine bado wapo zama za miswaki ya miti na dawa ya mswaki majivu au unga wa mkaa
 
YouTube. Huu ni mtandao ambao wengi wanaufahamu. Ni sehemu haswa rahisi ya kuingia na kutazama sinema unayoihitaji. Ni sehemu nzuri ya kuangalia ingizo jipya la filamu na matangazo ya sinema mpya. You Tube wana sinema ambazo unaweza kuangalia kwa malipo na zile utakazotazama bila malipo.
 
Tubi TV. Ukiwa kwenye mtandao huu utabaini kwamba kuna maelfu ya filamu za kisasa lakini zaidi zina sinema na TV Shows (vipindi vya runinga) ambavyo vimetayarishwa na watu maarufu kote duniani lakini baadhi ya hivi vipindi unaweza kuangalia bure na vingi ni vile vinavyokodishwa kwa malipo.
 
Top Documentary Films. Ikiwa wewe ni shabiki wa makala mbalimbali unaweza kuziangalia kupitia mtandao huu, makala hizi zinaangazia teknolojia, masuala ya kijamii, sayansi, siasa, siri, historia, mipango, mazingira, burudani na makala mbalimbali za uzipendazo.
 
Movies Found Online.com .Mtandao huu umeorodhesha sinema zote za bure za mtandaoni na hapa zimeorodheshwa wote katika mtandao mmoja na aina moja pamoja na mwaka wa kutolewa, unaweza kutazama filamu zilizoongezwa siku za karibuni kupitia mtandao huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…