Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NAPOLI YAMFUKUZIA KIUNGO WA CITY


Napoli itaanza upya jitihada za kumsajili kiungo wa Manchester City Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .
Zinchenko alijiunga na City mwaka 2016, lakini msimu uliopita alikuwa akitumika kwa mkopo PSV kabla ya kuivutia Napoli majira ya joto.
 
PSG YAMFUATILIA DIARRA


Paris Saint-Germain wapo kwenye mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Lassana Diarra, kwa mujibu wa SFR Sport .
Diarra kwa sasa anaichezea klabu ya Al Jazira ya Falme za Kiarabu, lakini anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure Januari.
 
MAN UNITED YACHUANA NA REAL KUMPATA HAZARD


Manchester United wamejipanga kupigana vikumbo na Real Madrid kwa ajiliya saini ya Eden Hazard, kwa mujibu wa Sun .
Hazard na bosi wa United wamefanya kazi pamoja wakiwa Chelsea, na kufanikiwa kunyanyua taji la Ligi Kuu msimu wa 2014-15.
Na gazeti hilo limedai kuwa United watatoa dau la paundi milioni 90 kwa ajili ya mchezaji huyo msimu ujao.
 
SPURS YAMTENGEA DAU NONO SUAREZ


Tottenham wanaandaa dau nono kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, kwa mujibu wa Don Balon .
Spurs wanaamini Barcelona watakuwa tayari kumuuza Suarez kwani wanalenga kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, na miamba hao wa London wameshaanza mazungumzona wawakilishi wa mchezaji huyo.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anasita kuondoka Camp Nou licha ya kuongezeka ushindani wa namba.
 
LEMAR ANAPENDA KWENDA LIVERPOOL

Nyota wa Monaco Thomas Lemar anapendelea kwenda Liverpool kuliko Arsenal dirisha la uhamisho wa Januari kwa mujibu wa The Independent .
Arsenal walishindwa kukamilisha dili la £90 milioni kwa ajili ya Lemar majira ya joto na inaaminika wanajipanga upya kumsajili winga huyo uhamisho wa Januari, Chelsea nao wakionyesha nia kumsajili.
 
REAL YASAKA MNUNUZI WA RONALDO


Real Madrid ipo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo ikiwa itatokea timu yenye dau nono Diario Gol .
Licha ya kuendelea kuongeza mataji kwenye klabu hiyo ya Hispania, kuna hisia ndani ya Santiago Bernabeu kuwa Mreno huyo nguvu zake zinaanza kufifia.
 
MAN UTD YAMWONGEZA KLUIVERT KWENYE ORODHA


Manchester United wamemwingiza Justin Kluivert kwenye orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Yahoo Sport .
Kinda huyo wa miaka 18 mtoto wa gwiji la Kidachi Patrick amebakiwa na miezi 18 kwenye mkataba wake, lakini Thomas Lemar, Malcom na Christian Pulisic pia wameingia kwenye rada kwani Jose Mourinho anataka kusajili winga mpya kwenye kikosi chake.
 
SALAH ANATAKA KWENDA REAL


Mohamed Salah anatamani kuihama Liverpool ili aweze kujiunga na Real Madrid, kwa mujibu wa habari kutoka Don Balon .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri amekuwa kwenye kiwango cha kutosha tangu alipotua Anfield majira ya joto, na timu nying kubwa za Ulaya zimeona na kuvutiwa na jitihada zake.
Miamba wa La Liga Real Madrid inaaminika ni miongoni mwa timu zilizopanga foleni kuiwania saini ya nyota huyo wa Kimisri.
 
POCHETTINO ANATAKIWA PSG


Paris Saint-Germain tayari wamegeuzia macho yao kwa meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, kwa mujibu wa The Mirror .
Miamba hao wa Ufaransa wanatarajia kumtema Unai Emery mwisho wa msimu huu kwani wanataka kumpata kocha mwenye wasifu mkubwa.
Pochettino ana vigezo vyote vya kuwa meneja katika Par des Princes, baada ya Mwargentina huyo kufanya vizuri Uingereza akiwa na Southampton na Spurs.
 
MAN UTD YATAJA BEKI YA MKHITARYAN


Manchester United wanahitaji kitita cha paundi milioni 35 kumuuza Mkhitaryan kwa mkataba wa kudumu uhamisho wa Januari kwa mujibu wa Daily Mail .
Inaaminika kuwa Inter wanaongoza katika mbio za kuifukuzia sainia ya kiungo huyo ambaye Mourinho hamkubali tena, lakini pia inawezekana Mwarmenia huyo kurudi zake Borussia Dortmund.
Mkataba wa mkopo unatarajiwa kuwa uwezekano mkubwa lakini United wapo tayari kumuuza kama dau nono likitolewa.
 
FELLAINI HATASAINI MKATABA MAN UNITED


Marouane Fellaini amejipanga kuondoka Manchester United kwani amekataa kusaini mkataba mpya klabuni hapo, kwa mujibu wa Express Sport .
Kiungo huyo ameshakataa ofa mpya tayari, na anataka kuondoka iwe ni Januari au mkataba wake utakapokwisha majira ya joto.
 
KLABU ZA EPL ZAMWANIA CARRASCO


Klabu za Uingereza zimepata fununu kuwa huenda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anaweza kumruhusu kuondoka winga wake Yannick Carrasco, kwa mujibu wa AS.
Manchester United na Chelsea zimetajwa kwenye tetesi za kutaka kumsajili Mbelgiji huyo miezi ya hivi karibuni, Mkataba wa Carrasco una thamani ya £86 milioni.
 
SPURS WATAVUNJA BENKI KUMBAKISHA KANE


Tottenham wamedhamiria kusambaratisha bajeti yao ili kuweza kumbakisha Harry Kane kwenye klabu yao, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa kinara wa mabao 2017 akifunga magoli 56, kwa sasa analipwa £110,000 kwa wiki kiasi ambacho ni kidogo kwa wachezaji wa kaliba yake.
Mshahara wa Kane utakuwa unaongezeka kwa mara ya nne tangu Agosti 2014, Spurs wakilenga kuzipindua ofa za Real Madrid.
 
PSG YAMFUATILIA DIARRA


Paris Saint-Germain wapo kwenye mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Lassana Diarra, kwa mujibu wa SFR Sport .
Diarra kwa sasa anaichezea klabu ya Al Jazira ya Falme za Kiarabu, lakini anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure Januari.
 
MAN UTD YAJITOA KWENYE MBIO ZA GRIEZMANN

Njia itakuwa nyeupe kwa Barcelona kumsajili Antoine Griezmann kwa kitita cha paundi £89 milioni kwani Manchester United hawatafanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid kwa mujibu wa Marca .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…