Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huimarisha Mifupa

Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi kwenye zabibu, na madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya. Kula zabibu mara kwa mara inasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri kuwa mkubwa. Pamoja na kuimarisha mifupa, madini haya husaidia mwili kufanya kazi vizuri.
 
Hulinda Dhidi ya Magonjwa ya Moyo

Zabibu huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu na ina kampaundi za flavonoids aina za resveratrol na quercetin ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Haya yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo na shinikizo la damu.
 
Kusafisha Figo

Zabibu zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo, pia hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mokojo unaotengenezwa na figo.
 
Kupunguza Lehemu (cholesterol)

Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu kwenye damu. Zina kampaundi kama pterostilbene ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza unywonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo.
 
Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani

Kama tulivyoona hapo juu kampaundi zinazopatikana ndani ya zabibu kama resveratrol ambazo husaidia kuondoa sumu zinazoweza kuleta saratani mwilini. Baadhi ya kampaundi nyingine huzuia seli za saratani kukua na kuzaliana; kuimarisha mfumo wa kinga wa mwili.
 
ni ndoto ya kila binadamu kuishi maisha marefu na yenye afya, kimsingi hakuna binadamu angependa kuishi maisha mafupi na yenye afya mbovu lakini kulingana na asili ya dunia yetu kuna changamoto nyingi sana za magonjwa na ajali ambazo zimepunguza urefu wa maisha wa binadamu wengi.vipo vyanzo vya vichache vifo ambavyo kimsingi haviepukiki lakini vyanzo vingi vinaweza kuepukika na kuongeza urefu wa maisha yako hapa duniani. yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuishi maisha marefu.
 
acha ulevi; unywaji wa pombe kupita kiasi una madhara makubwa kwa binadamu. madhara ya kifedha yaani kufilisika na na madhara ya kiafya. pombe ina haribu maini kwa kiasi kikubwa sana na baadae heleta kansa ya ini ambayo imeua vijana wengi wadogo.kama unapenda pombe basi kunywa kiasi kidogo na nyakati maalumu na haitakudhuru. lakini pia wasichana wengi wamejikuta wakifanya ngono mpaka na watu ambao hawakuwategemea sababu ya ulevi.
 
acha ngono zembe; tabia ya kufanya ngono na wanawake tofauti bila kinga haitakufikisha mbali, ukimwi umeua vijana wengi sana na sio rahisi kujua kwani hua ni siri ya familia siku ya mazishi na kama huwezi kutumia kondom basi tafuta mpenzi mmoja muaminifu na utulie naye.utafiti unaonyesha wanawake wmeathirika sana na ukimwi, pamoja na sababu zingine za kitaalamu lakini hofu yao ya mimba ni kubwa sana kuliko ukimwi.
 
kula vizuri; hakikisha kabla hujala chakula chochote unatafakari kama kina faida yeyote kwenye mwili wako, ulaji wa vyakula ambavyo havina faida mwilini kama pipi, biscuit, soda, na jamii zake vitakuua na kansa siku za usoni lakini pia unene ambao kimsingi huletwa na kula sana utakuletea magonjwa hatari kama kisukari na magonjwa mengine ya moyo.
 
tumia vyombo vya moto kwa uangalifu; matumizi ya vitu kama gari na pikipiki yanahitaji umakini mkubwa sana hasa ukiwepo barabarani, vijana wengi wadogo wameuawa na vyombo hivi.epuka kuendesha gari umelewa, epuka mwendo mkali, vaa helmet wakati wa kuendesha pikipiki, vunga mkanda wewe dereva au abiria na usikubali kubebwa kwenye gari au pikipiki na mtu ambaye hathamini maisha yake.usione aibu kumwambia dereva apunguze mwendo kwani umemlipa na ameshika maisha yako. na wewe usiyejua kuvitumia kajifunze kwanza chuoni ndio uanze kuvitumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…