shiriki mazoezi; magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa kama kisukari, ugonjwa wa moyo, na presha husababishwa sana na maisha ya uvivu. binadamu anatakiwa afanye mazoezi angalau nusu saa kwa siku. visingizio kwamba uko bize sana ni dalili ya kukosa vipaumbele na nidhamu kwenye maisha yako.hizo hela unazotafuta usiku na mchana usipokua na afya bora utakufa uziache.
epuka ugomvi usio na maana; mimi nafahamu watu waliopigwa ngumi moja tu wakafa hapohapo. mwili wa binadamu ni mlaini sana. kuna sehemu ambazo zikipigwa unakufa hapohapo. jitahidi kua mtu wa kusuluhisha zaidi kuliko kukunja ngumi.watu wote waliouawa kwa kuchoma visu au kupigwa mawe walikufa kwenye mazingira haya.kama umejifunza kupigana basi pigana pale unapokua umeshambuliwa ili kujilinda sio kuanzisha ugomvi makusudi.
usivute sigara; sigara ni moja ya starehe ambayo haina faida yeyote kwenye mwili wa binadamu, huharibu seli za kwenye mapafu na baadae huleta kansa ya mapafu.unaeza ukasema mbona fulani kavuta mapak leo hajafa. kila mtu ana kinga yake ya mwili amabyo ni tofauti na mwingine lakini pia hakuna anayechoka kuishi...huyo unayemuona anatamba, siku akiambiwa sigara ndio iko inamuua hata kama ana miaka 90 atasikitika sana.
usijihusishe na madawa ya kulevya; madawa ya kulevya hayatakuua hapohapo lakini yatakuondoa kwenye mkondo wa maisha ya mafanikio. utadharaulika na kila mtu, utakua huwezi kufanya kazi, muda mwingi utawaza kuiba ili upate madawa mengine ya kutumia.rafiki yangu mmoja mwaka 2004 alivuta bangi kwa kama miezi sita tu akawa kichaa na hajapona mpaka leo pamoja na kupelekwa hospitali nyingi za vichaa.unaweza ukaona jinsi amegeuka mzigo kwa ndugu zake.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitoza faini ya Sh100 milioni kampuni ya Star Media kwa kuwatoza fedha watazamaji wa chaneli zinazotakiwa kuonekana bila kulipiwa kupitia king’amuzi cha Star Times.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema kitendo hicho ni kinyume cha kanuni ya 14(2) (a) ya kanuni za Digital and Broadicasting Networks za mwaka 2011.
TCRA inaendelea kufuatilia kuhakikisha kuwa ving’amuzi vya Star Times, Continental, Digitek na Ting vinaendelea kuonyesha chaneli zote za kitaifa za FTA (Free to Air) bure kwa mujibu wa sheria,” alisema Kilaba.
Chaneli zinazotakiwa kuonekana bila kulipiwa ni TBC1, ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na Clouds TV. Kampuni hiyo imetozwa faini kuanzia Desemba 22 na inatakiwa kuwa imelipa kabla ya Januari 30.