Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia elimu hutolewa kwa ajili ya kuepuka mambo yanayoongeza presha tumboni kama mazoezi na michezo mikali yenye uwezekano wa kusababisha kuvuja au kupasuka kwa bandama.
Pia wagonjwa wanashauriwa kuvaa mkanda wanapoendesha gari ili kuepuka kupasuka kwa bandama iwapo itatokea ajali.
 
KWA WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU.

Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa maji maji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutoka na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu
 
Unaweza kufanya yafuatayo kujitibu mwenye kabla ya kumuona daktari
Nyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo wakati umelala kwa muda wa dakika 30 ili kuwezesha damu ya kutosha kurudi kwenye moyo. Fanya hivi walau mara 3 kwa siku kupata matokeo bora zaidi
 
Nyama zikiwa ndogo huwa hakuna dalili wala ishara zozote zinazoingilia mfumo wa upumuaji ila zinapokuwa kubwa uzuia hewa kuingia na kuharibu mfumo wa upumuaji sambamba na kushindwa kunusa, maumivu ya uso, maumivu ya meno ya juu, mafua, kukoroma, macho kuwasha na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa.
 
Dawa kama nasonex, cetirizine, antibiotiks huweza kutumika kwa nyia ya kunyunyuzia kwenye pua, vidonge au sindando ili kupuguza na kuzuia ukuaji wa nyama hizi huku zikisafisha mfumo wa upumuaji.
 
Upasuaji ufanyika endapo dawa zimeshindwa kuondoa tatizo ili na huwa ni upasuaji wa kutumia hadubini ya ndani kumuongoza daktari kuona kwenye njia ya hewa na miazi ya pua. Baada ya kufanya upasuaji utaweza kutumia dawa zilizotajwa juu hapo ili kuzuia kutokea tena kwa tatizo.
 
Back
Top Bottom