Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ule uwezo ulionao ndani mwako ni mkubwa vya kutosha kama utaamua kuutumia na kuweza kufikia ndoto zako. Huna haja ya kujitilia shaka kwamba hivi kweli mimi nitaweza, ndio unaweza, chukua hatua utaona matokeo yake.
 
Kama kuna watu wanakusema kwa sabau ya wewe kushindwa, acha waendelea kusema wao ni binadamu na wewe ni binadamu pia, chochote kinaweza kutokea kwenye maisha wasamehe bure, badili maisha yako na kuwa mwingine kabisa.
 
Kama hujui ni kivipi utabadilisha uwezo wako ulionao ndani mwako na kuweza kukubadilishia maisha yako, endelea kujifunza wakati unafika utajua. Wewe ni binadamu jifunze na utabadilika tu bila pingamizi lolote.
 
Tunajua mawe, udongo, milima ni vitu ambavyo havibadiliki, lakini wewe ni binadamu, usikalili maisha yako yawe hivyo hivyo milele , utakuwa unajizulumu sana. Maisha yako yana haki ya kupiga hatua, usijizuie kwa kusema aah mimi siwezi tena.
 
Acha kuishi kwa ndoto na kujisemea mimi mbona maisha yako ya hivivi tu siku zote, wewee, utakuwa unajidanganya na kujipoteza. Unao utajiri mkubwa ndani yako, jenga subira wakati utajiri huo unaousubiri kufumuka mbeleni unakuja.
 
Watu wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka mipaka katika kitu hicho pekee.
 
Watu wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka mipaka katika kitu hicho pekee.
 
Ukweli haipo hivyo hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi kutengeneza six park kwa kufanya mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali unaweza kutengeza six park kwa kufanya mazoezi ya aina tofauti tofauti.
 
Kwa muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate wako wa kila siku.
 
Hata mwandishi mmoja aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get what you always gotten” hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale ambayo umekuwa ukifanya siku zote, utapata yale yele ambayo siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena aya hii ili uielewe vizuri.
 
Kwani aya hiyo ipo wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi matokeo yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya iana tofauti na uliyoyazoea, unachotakiwa kufanya kubomoa uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda mambo yako ya msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako kwani binafsi naamini una kitu kingine cha kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.
 
Mwisho nimalizie makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako ya msingi acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa nyingine, bali unachotakiwa kufanya ni kubomoa uzio huo ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani pindi unavyoacha ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na mwisho wa siku kuelekea jehenamu ya umasikini.
 
Narudia kwa kusema tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya umaskini. Usiogope na kusema afisa mipango anakutisha hapana, ila kazi yangu ni kukwambia ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni kuwaza ni namna gani utaweza kufika mbali zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…