Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KUNYONYA KIDOLE KWA WATOTO

Kwa watoto wadogo, kunyonya kidole ni kitu kama cha kawaida vile, ingawa ni kwa watoto wadogo tu, wakati mwingine kunyonya kidole ni njia ya kumfanya mtoto apunguze njaa, ajibembeleze na kujisikia salama,mara nyingi mtoto ataacha kunyonya kidole akiwa na umri wa miaka 3-6.
 
Hebu tujiulize kwa nini mtoto anyonye kidole?

Kwa watoto wengi wananyonya kidole kama mbadala wa kula chakula, au kupembelezwa na wakati mwingine ni kujiweka au kujisikia salama, ni kama tabia tu, ambayo mtoto alikuwa nayo tangu akiwa tumboni kwa mama yake, mara nyingi kunyonya kidole kunaletwa na hisia.
 
Kama mtoto atashindwa acha kunyonya kidole mpaka baada ya miaka 5, kuna uwezekanao mkubwa wa meno yake kutojipanga vizuri, kuota yamebebana, na kupata meno yanayo shindwa kungatana.
 
Jinsi ya kumsaidia mtoto ili aache kunyonya kidole.

Wazazi huwa wanapata wasiwasi mapema pale mtoto anaposhindwa kuacha kunyonya kidole
 
Inashauriwa kuwa usimfanye mtoto aache kunyonya kidole akiwa na umri chini ya miaka 4 isipokuwa tu pale utakapoona kuna tatizo linalojitokeza kwa sababu ya kunyonya kwake kidole.
 
Back
Top Bottom