Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

629756915d113b3c613c2eed61a3cfc9.jpg
 
Hahahaha kaka ukihitajika sentro kesho shauri yako
Bageshi. Sentro tena? Mimi naongelea safari ya maisha yetu hapa duniani katika upana wake. Sekunde hii hii ninapoandika hapa sayari yetu hii inasafiri kwa kasi sana kujizungusha katika mhimili wake na kulizunguka jua pia. Nasi tumefumwa mumo kwa mumo katika safari hii ndefu ya mabilioni ya miaka, japo tunaishi kitambo kidogo sana katika muda wa kimalimwengu. Tumefumwa katika mfumo wa muda ambao daima huenda mbele na kamwe haurudi nyuma. Kwa vile sisi muda wetu una kikomo, kila sekunde inayogonga tunasogea katika ukomo wetu. Ndiyo maana nikasema nasi tumeshika kasi kuelekea kusikojulikana. Pengine kaburini. Pengine mbinguni. Pengine kuzimu. Hakuna ajuaye kwa uhakika. Hata hao watu wa sentro nao ni wasafiri tu katika safari hii ndefu tata na yenye kuchosha. Na mwisho wa yote haijalishi sana. Na kama alivyohitimisha Mfalme Suleiman yote ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.

Wakinipeleka sentro maelezo haya ndiyo nitayaandika katika utetezi wangu. Unafikiri wataniachia au ndo kwanza nitakuwa najichimbia kaburi? Binadamu !!!

Heri ya Mwaka Mpya bageshi !!!
 
Back
Top Bottom