Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mabula alieleza kuwa mwanamke yeyote anaweza kuzaa mapacha hata kama kwenye familia yao hakuna mtu aliyewahi kuzaa mapacha. Mtaalamu huyo wa afya alisema baadhi ya wanasayansi wanadai mbegu ya kiume ikiwa na nguvu kubwa husababisha kuvunjika kwa yai na kusababisha mapacha.
 
Aidha alishauri kuwa ili mwanamke kuweza kuwa na mimba yenye afya na kupata matokeo mazuri anayoyahitaji, aache kabisa au apunguze kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. Lakini pia, ili mwanamke ashike ujauzito kiurahisi tendo la ndoa linapaswa kuwa na maujuzi ili kulifurahia na kupata matokeo mazuri.
 
Wenzi wenye matatizo ya kutopata mtoto ambao vipimo vyao havionyeshi tatizo basi wanakosea namna ya kufanya tendo la ndoa,” alisema Dr. Mabula alipokuwa akitoa elimu hiyo kupitia kipindi cha Elimika Wikiendi ambacho hufanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi kupitia mtandao wa Twitter.
 
Matumizi ya magnesiamu, kalsiamu. Dr. Mabuli alitahadharisha kuwa, matumizi hayo huongeza uwezekano wa kupata mtoto wa jinsia ya kike.
Kupandikiza maabara mbegu za kiume na mayai kisha kuyahamishia kwa mwanamke. Upandikizaji huongeza fursa ya kupata mapacha kwa maana kiinitete zaidi kimoja kinaweza kuhamishwa baada ya kurutubishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…