Maisha ya jamaa huyu kwa kweli ni kama filamu. Ni ya kushangaza. Yanaweza kuunda filamu nzuri sana," amesema Wenger.
"Nakumbuka nilipomuona mara ya kwanza Monaco alipofika na alikuwa anaonekana kukanganyikiwa kidogo, hakuwa anamjua mtu yeyote, na hakuwa anatazamwa na wengi kama mchezaji stadi na baadaye akaibuka na kuwa mchezaji bora duniani 1995 na leo hii sasa amekuwa rais wan chi. Ni kisa cha kushangaza," Wenger ameongeza.