Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ziara hiyo imefanyika wakati vyama vya siasa vikijiandaa kuanza kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ambao ni wa kwanza tangu Robert Mugabe ang’atuke madarakani kwa shinikizo la jeshi.
 
Mnangagwa, ambaye aliongozana na makamu wake Constantino Chiwenga, mkuu wa zamani wa jeshi aliyeongoza mapinduzi ya kimyakimya Novemba mwaka huu, alisema Tsvangirai anaendelea “kupata ahueni". Tsvangirai aligundulika kuwa na kansa ya utumbo mpana miaka miwili iliyopita
 
Makamu wa Tsvangirai katika chama cha Movement for Democratic Change (MDC), Nelson Chamisa alisema kitendo alichofanya Mnangagwa ni ishara ya upendo ambayo “tunahitaji kuona katika siasa nchini". "Siasa za amani, siasa za kufanya kazi pamoja, siasa za kujuliana hali," alisema.
 
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 Tsvangirai alipata kura nyingi dhidi ya Mugabe lakini hazikutosha kuepuka uchaguzi wa marudio. Wafuasi wa Mugabe walipoendesha vurugu dhidi ya wafuasi wa MDC, Tsvangirai alijiondoa na baadaye aliingia katika majadiliano na serikali, akakubali mpango wa kugawana madaraka yeye akiteuliwa kuwa waziri mkuu.
 
Kama mojawapo ya mkakati wa kutekeleza dhamira hiyo, Serikali ya Awamu ya Tano imeanzisha mkakati wa ujenzi wa viwanda.

Ni mkakati ambao aghalabu umekuwa ukitajwa na viongozi katika majukwaa mbalimbali na hilo ni kwa sababu viwanda ndio mwelekeo wa Serikali yetu kiuchumi.
 
Katika safari hii ya Tanzania ya viwanda, pamoja na ukweli kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa namna yake, kwetu sisi msisitizo mkubwa tunauweka katika uwekezaji na uimarishaji wa vyombo ambavyo tayari vimeshajipambanua kama waendelezaji wa viwanda nchini.
 
Mojawapo ya vyombo hivyo ni Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido).

Kwa muda mrefu sasa, Sido imekuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo na kubuni mashine rahisi zinazotumiwa na wajasiriamali wengi nchini walioanzisha viwanda vidogo na vile vya kati.
 
Kwa kufanya hivyo, chombo hiki kimekuwa kikichochea ajira kwa wananchi na kuwa msingi wa kukuza uchumi, maendeleo ya nchi na ustawi wa raia. Tunapohamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda kutoka kwa wawekezaji wa nje na wa ndani, chombo kama Sido hakina budi kutazamwa kwa jicho la karibu, kwa kuwa ndio mkombozi wa wananchi.
 
Kwa kukitumia chombo hiki, wananchi wanaweza kuanzisha viwanda vingi vidogo, vya kati na hatimaye viwanda vikubwa.

Inatia moyo kusikia kuwa mwaka huu, Serikali imeitengea Sido jumla ya Sh5.5 bilioni, fedha ambazo pamoja na mambo mengine, uongozi wa shirika hilo unasema utazitumia kujenga ofisi mpya na kuziboresha zile za zamani.
 
Tunaamini ikiwa Sido itajengewa uwezo kama huu, bila shaka itajikita katika kazi ya kutoa mafunzo ya utengenezaji wa zana rahisi za uzalishaji na uchakataji wa mazao, jambo litakalofanya safari ya kuiendea Tanzania ya viwanda kuwa na mafanikio makubwa.
 
Katika kilimo kwa mfano, tumekuwa tukiona mashine nyingi rahisi zikitumika katika nchi nyingine. Hizi zikizalishwa kwa wingi nchini sio tu zitavutia wengi kuingia katika shughuli za kilimo, lakini uzalishaji wa mazao mbalimbali utaongezeka.
 
Katika kilimo kwa mfano, tumekuwa tukiona mashine nyingi rahisi zikitumika katika nchi nyingine. Hizi zikizalishwa kwa wingi nchini sio tu zitavutia wengi kuingia katika shughuli za kilimo, lakini uzalishaji wa mazao mbalimbali utaongezeka.
 
Kukua kwa uzalishaji wa kilimo unaotokana na Watanzania kulima kwa teknolojia na mashine za kisasa, kunamaanisha viwanda vitakavyoanzishwa vitakuwa na uhakika wa kupata malighafi.

Tunasisitiza kuwa ili ajenda ya kuelekea Tanzania ya viwanda iwe na mashiko, vyombo kama Sido havipaswi kupewa kisogo. Huko ndiko kwenye chimbuko la viwanda vidogo ambavyo kwa uzoefu Watanzania wanaweza kuvimudu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…