Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Icardi & Kane kwenye rada za Real Madrid


Mauro Icardi na Harry Kane ni wachezaji wanaopewa nafasi kubwa kusajiliwa na Real Madrid ili kuimarisha safu yao ya mashambulizi, kimeripoti Diario Gol.
Icardi wa Inter anatarajiwa kusajiliwa uhamisho wa Januari, wakati Kane akiwekewa malengo ya majira ya joto.
 
Rafa aambiwa lazima auze wachezaji Newcastle


Rafa Benitez ameambiwa kwamba ni lazima auze kwanza kabla ya kutaka kusajili wachezaji wapya Newcastle, kwa mujibu wa Sun.
Kutowekeza vya kutosha kwenye kikosi kumekuwa lalamiko la muda mrefu kwa Muhispania huyo tangu alipowarejesha Megpies Premier League.
 
Monaco yafungua mlango wazi kwa Lemar


Kocha mkuu wa Monaco Leonardo Jardim amekubali kwamba itakuwa kazi nzito kwake kumbakisha Thomas Lemar klabuni mwake uhamisho wa Januari.
"Hatuna desturi ya kuuza majira ya baridi," Jardim aliwaambia waandishi Jumatatu. "Lakini dirisha la uhamisho litafungwa mwishoni mwa mwezi huu na mambo mengi yanaweza kutokea."
 
Barca yafanikiwa kumpata kwa €11.5m Mina


Barcelona wamekubali kutoa €11.5 milioni kumnunua Yerry Mina kutoka Palmeiras Sport.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa chanzo cha vita kali baina ya Catalan na Wabrazili hao wiki za hivi karibuni. Mina anatarajiwa kutua Barcelona kukamilisha uhamisho wake wiki hii.
 
Mourinho aiambia Man Utd: Nunua Kante au nasepa


Jose Mourinho ameitaka Manchester United kumsajili N'Golo Kante ikiwa wanataka aendelee kuinoa klabu hiyo, kwa mujibu wa Don Balon.
Nyota huyo wa Chelsea anaaminika kuwa kiungo bora zaidi mkabaji duniani na Jose Mourinho anamhusudu mno.
 
Fellaini anataka kuondoka Man United


Marouane Fellaini amemwambia Jose Mourinho kwamba havutiwi kuendelea kubaki Manchester United, kwa mujibu wa Sun.
Kiungo huyo wa Kibelgiji, ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha msimu huu, anamaliza mkataba wake majira ya joto.
Baada ya kukataa mkataba mpya mwezi Septemba amekataa kwa nguvu zote kushawishiwa na Mourinho kusaini mkataba mpya.
 
Bei ya Alex Sandro yaivuruga Chelsea


Jitihada za Chelsea kumsajili Alex Sandro zimeanza kuingiliwa na baada ya Juventus kuwake dau kubwa kwa ajili ya mchezaji huyo, kwa mujibu wa Telegraph.
Sandro amekuwa shabaha ya Antonio Conte kwa muda mrefu kwani anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi
Lakini Juve wamekomaa wanataka £60 milioni, ada ambayo Chelsea hawataki kutoa.
 
Chelsea, Arsenal & Man Utd zamwania Bailey



Chelsea, Manchester United na Arsenal zinataka kuingia vitani kuwania saini ya Leon Bailey, kwa mujibu wa Mirror.
Winga huyo wa Leverkusen anaweza kupatikana kwa ada ya uhamisho ya kiasi cha £40 milioni, ingawa klabu inasita kumuuza.
 
Arsenal wanamtaka Lemar kwa £90m kumrithi Alexis



Thomas Lemar amerudi kwenye rada za Arsenal akitarajiwa kutua Emirates kuchukua nafasi ya Alexis Sanchez anayetazamiwa kwenda Man City, kwa mujibu wa Mirror.
 
Man City kumnasa Alexis Sanchez wiki hii

Uhamisho wa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwenda Manchester City unaweza kukamilika mapema wiki hii, kwa mujibu wa Express .
City wameonyesha nia ya kumsajili mchezaji wa zamani wa Pep Guardiola akiwa Barca mwezi Januari, na klabu hizo mbili zipo kwenye mazungumzo.
Vinara hao wa Ligi Kuu Uingereza wanataka kukamilisha usajili huo haraka iwezekanavyo, na wanatumai kumsajili Alexis kwa ada ya uhamisho ya £30 milioni.
 
Timu ya daraja la chini Yeovil Town imepangwa na Manchester United kwenye raundi ya 4 ya kombe la FA
Timu hiyo ambayo ipo daraja la pili ilifanikiwa kuiondoa klabu ya Bradford City kwa magoli 2-0 wikendi iliyopita na sasa watawakaribisha United kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Huish Park mwishoni mwa mwezi huu
Pia klabu nyingine ya daraja la chini ya Newport Country, ambao waliwaondoa Leeds United nao watavaana dhidi ya Tottenham mechi ambayo inatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Newport
Aidha Liverpool nayo imepangwa na West Bromwich Albion mechi itakayo pigwa kwenye dimba la Anfield, wakati Chelsea ambaye bado ana mchezo wa marudiano dhidi ya Norwich, anatarajiwa kukutana na Newcastle endapo atashinda mechi ya marudiano
Vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Manchester City wao wana msubiri mmoja wapo kati ya Cardiff City au Mansfield Town, huku wababe wa Arsenal klabu ya Nottingham Forest watavaana na Hull City
 
Droo yote ya FA Cup kama ifuatavyo
Liverpool v West Brom
Peterborough v Fleetwood/Leicester
Huddersfield v Birmingham
Notts County v Wolves/Swansea
Yeovil v Manchester United
Carlisle/Sheffield Wednesday v Stevenage/Reading
Cardiff/Mansfield v Manchester City
MK Dons v Coventry
Millwall v Rochdale
Southampton v Watford
Middlesbrough v Brighton/Crystal Palace
Bournemouth/Wigan v Shrewsbury/West Ham
Hull v Nottingham Forest
Newport County v Tottenham
Norwich/Chelsea v Newcastle
Sheffield United v Preston
 
Back
Top Bottom