''Nimejitahidi kutoruhusu presha kutoka nje na ndani ya klabu kwasababu najua ipo siku nitaacha kufundisha hapa, siwezi kuwa hapa kwa miaka 10, najitahidi kutumia muda wangu kufanya kila kitu kwaajili ya klabu'', amesema Zidane kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Runinga nchini Ufaransa ambako ameenda kwa mapumziko mafupi.