Nikiwa makamu wa rais na msaidizi mkuu, nawasihi viongozi wote wa Jubilee wampe rais nafasi kuunda serikali. Hakuna mwenye mamlaka ya kumsimamia rais katika wajibu wake wa kikatiba,” alisema Ruto.
Rais Kenyatta aliwarejesha mawaziri sita na akateua wapya watatu na akawaacha njiapanda wengine 13.
Moi akataa uwaziri
Katika hatua nyingine Seneta wa Baringo, Gideon Moi, Jumanne alitofautiana na watu wanaotaka apewe nafasi ya uwaziri katika serikali ya Rais Kenyatta akisema hata akipewa nafasi hiyo hataikubali kwa kuwa kwa sasa wajibu wake ni kuhudumia wakazi wa Baringo.