Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

26238911_1826193170747298_8943184585415138550_n.jpg
 
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku anazungumza na mawakili wake kuhusu madai yaliotolewa na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri kwamba aliamua kuondoka katika klabu hiyo baada ya kupata ''ujumbe wa uchawi''.
Moshiri aliuambia mkutano wa wamiliki wa hisa katika klabu hiyo kwamba Lukaku mwenye umri wa miaka 24 alipokea ujumbe huo baada ya kuzuru Afrika.
Lukaku alijiunga na United kwa pauni milioni 75 mwezi Julai baada ya kukataa kandarasi mpya Everton.
Mwakilishi wa mchezaji huyo aiambia BBC michezo kwamba uamuzi wa Lukaku haukushinikizwa na uchawi.
 
Msemaji huyo aliongezea: Hapendi kufuata imani kama hizo na sasa anatathmini hatua za kisheria anazoweza kuchukua.
BBC michezo inaelewa kwamba raia huyo wa Ubelgiji amekasirishwa na madai hayo.
Wawakilishi wake wanasema kuwa Lukaku alikataa kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu ya Everton ili kuweza kucheza katika klabu kubwa duniani.
Wawakilishi wake waliongezea: Romelu ni mfuasi wa kanisa katoliki na kwamba haamini uchawi. Hakuwa na imani na Everton mbali na mradi wa bwana Moshiri.
Hiyo ndio sababu hakutaka kutia kandarasi nyengine.
 
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa uamuzi wake wa kumchezesha Alexis Sanchez kama mchezaji wa ziada dhidi ya Chelsea siku ya Jumatano hauna uhusiano na uvumi kuhusu uhamisho wake na kusisitiza hamu yake ya mshambuliaji huyo kusalia katika kabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi Juni aliingia katika kipindi cha pili katika nusu fainali ya kombe la Carabao mkondo wa kwanza mbapo timu hizo zilitokare sare tasa.
Sanchez anahusishwa na uhamisho wa Manchester City mwezi huu.
''Nataka asalie kwa kipindi kirefu'',alisema Wenger. ''Sina tatizo iwapo atasaini kandarasi mpya nasi iwe sasa au mwezi Juni''.
Lazima ukubali wakati unapocheza mechi nyingi na Sanchez hucheza kila mechi, na kwamba wanapopimzika katikati ya msimu huwasaidia kidogo.
 
Licha ya utata unaokumba hatma ya Sanchez, Wenger haamini kwamba Sanchez anataka kuondoka.
''Watu hawamjui Sanchez- huyu ni mchezaji ambaye lengo lake kuu ni kucheza kandanda'', aliongezea Wenger.
''Unamuona alivyokuja leo, alijiandaa kama mchezaji anayetaka kucheza''.
 
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ameunga mkono utumizi wa mfumo wa video unaowasaidia marefa baada ya timu yake kutoka sare tasa na Arsenal katika nusu fainali ya kombe la Carabao mkondo wa kwanza.
Refa Martin Atkinson alitumia mfumo huo wa VAR kwa madai mawili ya penalti ya Chelsea wakati ambapo Victor Moses aligongana na Maitland-Niles katika kipindi cha kwanza na wakati Danny Welbeck alipomkabili Cesc Fabregas , na alifurahi kwamba ushahidi alioonyeshwa haukuwa wa kutoa panalti.
 
Nafurahia utumizi wa VAR kwa sababu kunapokuwa na wasiwasi wakati wa mechi ni vyema wakati refa na wasaidizi wake wanapoangalia video hiyo na kutoa uamuzi mwafaka'', alisema Conte.
''Nadhani kila mtu anataka makosa machache wakati wa mechi na nadhani hilo litasaidia sana''.
Timu hizo mbili zitakutana tena katika mkondo wa pili katika uwanja wa Emirates mnamo tarehe 24 mwezi Juni baada ya Arsenal kuonyesha ukakamavu kufuatia kushindwa kwao katika kombe la FA na klabu ya Nottingham Forest.
''Arsenal ilicheza vizuri'', alisema Wenger.
''Tulikuwa tumejiandaa na ilikuwa sare nzuri na sasa ni lazima kumaliza kazi tulioanza''.
 
Back
Top Bottom