Hayo yamebainika baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa kutembelea uwanja huo na kuliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pamoja na TAA kukaa na kuona ni kwa namna gani wataliondoa bomba hilo ambalo limeonekana kukwamisha shughuli za upanuzi wa uwanja.
“Kama nilivyosema hii haiwezi kukubalika, nirudie kusema TPDC na TAA na wataalamu wa wizara waje wakae lakini kikubwa waangalie namna ya kulitoa hili bomba kwa sababu hizi ndege zitakapokuwa zikishuka hapa wanaweza kufuta safari zake wakigundua kuna bomba la gesi na mimi ninavyojua bomba hili ni hatari,” amesema Kwandikwa