Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JUISI YA TENDE MAHITAJI : Tende kilo moja Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja Hiliki NAMNA YA KUTENGENEZA : Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake. Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine. Ziweke kwenye blenda na hiliki.Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda hadi zitakapolainika sawasawa. Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema. Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, Unaweza kuiweka kwenye friji ili ipate ubaridi au ukanywa hivo hivo sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.
 
MILKSHAKE YA NDIZI/BANANA MILKSHAKE:- MAHITAJI: 1.NDIZI ZA KUIVA 2 2.MAZIWA YA MAJI KIKOMBE KIMOJA 3.MDALASINI WA UNGA KIJIKO KIMOJA CHA CHAI 4.SUKARI KIJIKO KIMOJA CHA CHAKULA JINSI YA KUTENGENEZA:- 1.MENYA NDIZI VIZURI NA UZIKATE KATE UTIE KATIKA BLENDA 2.WEKA KATIKA BLENDA MAHITAJI YAKO MENGINE YOTE YALOBAKIA NA USAGE MPAKA VILAINIKE. 3.MIMINA NA UWEKE KATIKA GLASS/JAGI NA UTIE KATIKA FRIJI ILI IPATE UBARIDI KIDOGO NA HAPO ITAKUA TAYARI KWA KUNYWA.
 
JUICE YA UBUYU Mahitaji Ubuyu(wa unga au wa mbegu) Maji Sukari Njia: 1.Chambua ubuyu,ondo uchafu wowote uliopo kwenye ubuyu 2.Katika sufuria,weka ubuyu kisha ongeza maji.Katika kila kipimo cha ubuyu ongeza maji mara tatu yake Ubuyu wa mbegu vikombe 6 weka maji vikombe 9 Ubuyu wa unga vikombe 3 weka maji vikombe 12 3.Funika sufuria kisha bandika jikoni,chemsha adi vitokote,vipe angalau dakika nne za kutokotea. Kumbuka maji unayotumia kuchemsha ubuyu ni maji ya bomba na si salama,hivyo ni muhim kuyapa muda mzuri wa kuchemka ili juice yako iwe salama. 4.Juisiinapoanza tu kutokota ongeza sukari kwa ladha uipendayo kisha acha zile dakika nne za kutokota ziishe.Zima jiko acha juisi ipoe. Napenda kuweka sukari ichemkie kwenye juice kwani inafanya juice ishikane na kua nzito.Sukari ikichemshwa inakawaida ya kua nzito.Kumbuka kwamba ubuyu ni mwepesi sana na juice yake kawaida hujitenga inapotulia,ubuyu waenda chini na maji yanabaki juu.Ukichemsha sukari inasaidia kuondoa hali hiyo. 5.Chuja juisi,ongeza maji kama unaona ni nzito sana,na ongeza sukari endapo ile uliyoweka awali haitoshi.Juisi tayari kwa kunywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…