Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanga wa taa hizi humsaidia dereva kuona barabara vizuri wakati wa usiku lakini pia huwawezesha madereva na watumiaji wengine wa barabara kujua kuwa kuna gari linakuja.
 
1516109011377.jpg
 
Taa zenye mwanga mdogo hukuwezesha kuiona barabara na haiwaathiri madereva au watumiaji wengine wa barabara kutokana na kiwango kidogo cha mwanga wake. Wakati mwingine taa hizi hutumika hata mchana endapo kuna ukungu mkali ili kutoa ishara kwa watumiaji wengine wa barabara.
 
Unaweza kutumia taa zenye mwanga mkali endapo hakuna gari jingine au chombo kingine cha moto kinachokuja mbele yako. Kutokana na mwanga huo mkali, ukimpiga machoni dereva mwingine anaweza kupoteza uono na kushindwa kuongoza gari.
 
Watu wengi wanaofanya safari maeneo ya mijini hawapaswi kutumia taa hizi kutokana na uwepo wa magari mengi na pia hakuna giza tororo.
 
Taa za nyuma (Tail lights)
Taa hizi hutoa mwanga mwekundu upande wa nyuma wa gari na zimeunganishwa katika mfumo ambao utaziwasha wakati wowote ambao taa za mbele zimewashwa. Hii husaidia sana wakati wa giza dereva wa nyuma yako kutambua kwamba mbele yake kuna gari na atambue umbali uliopo baina ya gari lake na gari la mbele yake.
 
Taa za kutembelea mchana
Taa hizi hazipo katika magari yote, zinapatikana zaidi katika magari ya kisasa yaliyotengenezwa miaka ya hivi karibuni.
 
Taa hizi hupatikana katika maeneo yote ya nyuma na mbele ya gari na huwasha pale gari linapowashwa, japokuwa kwenye baadhi ya magari unaweza ukazizima.
 
Zimetengenezwa kutoa ishara na kukuwezesha wewe kuonekana zaidi na dereva anayekuja nyuma yako, lakini wengine hizizima kwa vile huona hazina maana sana. Baadhi ya watu huziacha ziwake kwani hutumika kama urembo wa kuongeza mvuto kwenye gari.
 
Taa za ukungu (Fog lights)
Taa hizi hupatikana karibu na taa za mbele. Kwa kawaida huwa zina mwanga mdogo ili kuzuia mwanga wake usiakisi katika ukungu na kukurudia wewe (dereva).
 
Zinatakiwa kutumika tu endapo kutakuwa na ukungu ili kutoa ishara kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara. Lakini madereva wengine huamua pia kutumia taa za mbele zenye mwanga mdogo kukiwa na ukungu.
 
Taa za ishara (signal Lights/ indicators)
Hizi hutumika zaidi katika kutoa ishara kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara. Zinapatikana nyuma, pembeni (sio magari yote) na mbele ya gari. Mara nyingi zinakuwa pembeni ya taa za mbele na taa za nyuma.
 
Taa hizi hutoa ishara kwa dereva mwingine kuwa unataka kuingia upande fulani. Ukiwasha taa za upande wa kushoto itamaanisha unataka kuingia upande wa kushoto, vivyo hivyo na upande wa kulia.
 
Back
Top Bottom