Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama unaegesha gari lako sehemu ambayo mbele kuna watu, si ustaarabu kuwamulika na taa yenye mwanga mkali, badala yake unawasha taa hii na inakupa mwanga kidogo kuwezesha kuegesha gari.
 
Baadhi ya watu huendesha magari yao taa hizi zikiwa zinawaka hata kama ni mchana, na kwenye baadhi ya magari zimetengenezwa kuwa kama urembo ambapo hutumika wakati wa mchana.
 
Taa zinazoashiria gari kurudi nyuma (Reverse lights)
Taa hizi zipo nyuma ya gari na huwaka kwa rangi ya kung’aa kama taa za mbele. Matumizi makubwa ya taa hizi ni wakati wa kurudisha gari nyuma.
 
Screenshot_2018-01-16-14-55-53.png
 
Taa hizi huwaka kwa mwanga mweupe ili kumuwezesha dereva kuona nyuma kwa ufasaha wakati gari likirudi nyuma hasa wakati wa usiku ama panapokuwa na mwanga hafifu.
 
Taa ya namba za gari (license plate lights)
Unapowasha gari taa za mbele za gari lako ili uweze kuona njia, taa hizi pia huwaka. Lengo kubwa la taa hizi ni kuonyesha namba ya usajili wa gari lako wakati wote.
 
Baadhi ya watu wakifanya uhalifu hukimbia wakitaka wasijulikane, lakini taa hizi zikiwa zinawaka, itawezekana kurekodiwa kwa namba za usajili wa gari lako kwa hatua zaidi.
 
Ni muhimu kuhakikisha kuwa taa zote kwenye gari lako zinawaka sawa sawa. Kuna baadhi ya taa ambazo kama hazifanyi kazi utatozwa faini lakini nyingine hautotozwa.
 
Taa za ndani ya gari na taa za ukungu si kosa kisheria kutokuwa nazo lakini ni muhimu kwa ajili ya kukurahisishisha kazi yako ya udereva
 
Kwenye upande wa taa za ukungu, sio magari yote yanazo, kwani tumeeleza awali kwamba baadhi ya madereva hutumia taa za kawaida.
 
Hakikisha unafanyia usafi taa zako kila mara ili kutoa mwanga wa kutosha na pia kuzibadilisha mara tu zipatapo tatizo.
 
Back
Top Bottom