Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JUICE YA MCHAI CHAI+TANGAWIZ UNAUSAFISHA MCHAI CHAI KISHA UNAKATAKATA ,UNAMENYA TANGAWIZI KISHA UNAKATA VIPANDE VIDOGO VIDOGO NA KUMIX NA MCHAI CHAI THEN TIA MAJI SAFI NA SSLAMA ,UKIPENDA KUTIA SUKARI PIA YAFAA KISHA UNA TIA KTK BRENDA NA KUSAGA THEN UNACHUJA,NI NZURI UKINYWA ILIOPOA
 
JINSI YA KUTENGEZA JUICE YA MCHANGANYIKO WA TIKITI NA LIMAO. MAHITAJI 450 grams Vipande vya Watermelon vyenye ubaridi, 250 gram ya maji ya dafu au Nazi changa 1 limao kubwa 10 vipande vya barafu au Ice cubes, Fresh Mint kwajili ya kupambia Kata nusu tikiti maji zuri lililoiva kama unavyoona kwenye picha kisha likate kate vipande na uweke kwenye friji vipoe kabla ya kutengeneza juisi yako Chukua maji ya dafu, limao, vipande vya barafu na vipande vya tikiti maji kisha weka kwenye blender. Lengo la kuweka limao ni kuongeza na kubalance ladha. kama wewe ni mpenzi sana wa maji ya madafu unaweza ongeza zaidi ili ladha ya madafu isikike sana. Blend vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike safi kabisa. Perfect drink for your summer, waandalie familia wafurahie pia kama unabiashara waandalie wateja wako wafurahie sana hasa kipindi hiki cha majira ya joto. kumbuka tikiti maji na dafu vyote vinasukari kwahiyo huna haja ya kuongeza sukari kabisa na ukafurahia kinywaji hiki murua.
 
JINSI YA KUANDAA YA KUTENGENEZA JUICE YA EMBE NA PASSION. Vipimo Passion fruit 8 Embe 6 za kiasi Maji kiasi Sukari kiasi upendavyo Namna Ya Kutyarisha 1. Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje . 2. Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion. 3. Tia sukari korogo ikiwa tayari
 
JINSI YA KUANDAA NA KUTENGENEZA SHARBATI YA STRAWBERRY NYUMBANI ( Strawberry Shake) VIPIMO Ndizi 2 Kiasi Stroberi (strawberries) 2 Vikombe vya chai Vipande vya barafu 1 Kikombe cha chai Maziwa ¾ − 1 Kikombe cha chai Juisi ya machungwa 1 Kikombe cha chai Asali 2 Vijiko vya supu NAMNA YA KUTAYARISHA 1. Kata kata ndizi na stroberi na uweke kwenye mashine (blender) pamoja na vipimo vyote vilivyobaki. 2. Saga hadi ilainike vizuri. 3. Mimina kwenye gilasi na ni vizuri kunywiwa hapo hapo.
 
Wataalamu wa afya wanasema kuwa mikate, chipsi na viazi vinatakiwa kupikwa mpaka viwe na rangi ya dhahabu (njano) badala ya kuwa rangi ya udongo ili usile tunakula kemikali aina ya Acrylamide yenye madhara inayoweza kusababisha saratani (kansa).
 
Kemikali hii inatoka kwenye chakula chenye wanga zaidi kama viazi na mikate zinapookwa au kukaangwa kwa joto la juu na kwa muda mrefu zaidi zinamsabababishia mlaji kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuugua kansa.
 
Shirika la viwango la chakula nchini Uingereza limependekeza wapishi kuwa makini kufuata maelekezo ya njia sahihi za kupikia na kuepukana na mitindo ya kudumisha rangi ya kahawia.
 
Pia shirika hilo limesema kuwa, viazi na mizizi inayofanana na karoti hazifai kuhifadhiwa kwenye friji. Hiyo ni kwa sababu viwango vya sukari hupanda katika mboga zikihifadhiwa katika joto la chini, hivyo kuwa na uwezekano wa kuongeza kiasi cha Acrylamide inayozalishwa wakati wa kupika chakula.
 
Kiwango cha juu zaidi cha Acrylamide hupatikana katika vyakula vya wanga ambavyo vimekuwa vikipikwa kwa joto la juu la sentigredi 120 kama vile chipsi, mikate, nafaka, biskuti, kahawa, n.k.
 
Utafiti uliofanywa kwa wanyama umeonesha kuwa kemikali hiyo ni sumu ambayo husababisha kansa, hivyo wanasayansi wanadhani kuwa kwa binadamu yawezekana ikawa na madhara hayo hayo.
 
Taa katika gari lako unaweza kuona ni kitu kinachotumika tu kukupatia mwanga, lakini kiukweli, taa katika gari ni muhimu kwani zinafanya kazi mbalimbali zaidi ya ile ya kutoa mwanga kama vile kutoa ishara ya muelekeo wa gari, hali ya gari na zaidi.
 
Unaweza kujikuta unatozwa faini kila mara, ukafungwa gerezani au kupata ulemavu na hata kifo (kutokana na ajali) endapo utashindwa kutumia kwa usahihi taa za gari lako.
 
Japokuwa inaweza kuonekana ni kitu kidogo na cha kawaida, lakini baadhi ya madereva hukumbwa na wakati mgumu kujua aina sahihi ya taa za kutumia katika eneo husika. Wengine hawafahamu hata aina mbalimbali za taa zilizopo katika gari, wengi wao wanajua taa za kumulika barabarani tu.
 
Katika makala ya leo, tutachambua aina mbalimbali za taa kwenye gari na matumizi yake.
 
Taa za mbele
Kuna aina mbili za taa za mbele, taa zenye mwanga mdogo (Low beam lights) na taa zenye mwanga mkali (High beam lights).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…