Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

26262304_162474837728622_1044576590878474240_n.jpg
 
Ajira au kazi katika ujumla wake huwakusanya pamoja watu wa tabia, haiba na mikabala mbalimbali ya kimaisha. Tabia na haiba hizi tofauti wakati mwingine huweza kusababisha misuguano , majuto na hata sononi. Kuna wakati bosi ni mkorofi na watumishi wengine wanakuwa wamekaa kisharishari tu.
 
Hali kama hizi ndizo huwafanya baadhi ya watumishi kusubiri likizo kwa hamu kubwa sana. Kwa kwenda likizo hujisahaulisha na vurugu hizi. Lakini wengine huamua kubadili ama kuacha kazi kabisa.
 
Hatua hizo mbili zinaweza kuwa ni za muda mfupi tu. likizo hatimaye huisha na mtu hurejea kazini au kule anakoenda baada ya kuacha sehemu ya awali, anaweza kupambana na kero kubwa na nyingi zaidi.
 
Nijuavyo mimi, kuna mambo ambayo mtu akiyafanya, vurugu na tafrani hizi za makazini haziwezi kumdhuru, bila kuhama au kwenda likizo.
 
Back
Top Bottom