Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unahitajika kuhakikisha mafuta lainishi (oil) yapo katika hali nzuri na katika kiwango cha kutosha katika injini yako. Pia unatakiwa kukagua ujazo wa magurudumu ya gari lako; kwani kadri gurudumu linavyokuwa na ujazo mdogo, ndivo linavyohitaji mafuta mengi zaidi kulizungusha.
 
1516384251796.jpg
 
Zingatia matuta

Matuta huwekwa katika barabara ili kutawala mwendo. Hivyo kufunga breki ghafla mara ukutapo tuta na kuchochea mwendo ghafla baada ya tuta kutakufanya utumie kiasi kikubwa zaidi cha mafuta.
 
Unaweza kupunguza mwendo taratibu na kuuongeza taratibu mara ufikapo kwenye matuta ili kuokoa kiasi cha mafuta kinachopotea.
 
Zima kiyoyozi

Ufanyaji kazi wa kiyoyozi (AC) katika magari mengi hutegemea nishati inayozalishwa na kifaa kiitwacho Alternator ambacho huzalisha umeme kwa msaada wa injini ya gari.
 
Hivyo basi, kuwasha kiyoyozi kutahitaji mafuta zaidi ili kuendesha kifaa hiki kiitwacho Alternator. Inashauriwa kuwasha kwa muda au kuzima kiyoyozi pale ambapo hakina ulazima ili kuokoa matumizi ya mafuta yasiyo ya lazima.
 
Tumia kiongeza mwendo vyema

Matumizi mazuri ya kiongeza mwendo (Accelerator), kutakuokolea kiasi kikubwa cha mafuta mara uendeshapo gari. Mambo ya kuzingatia katika swala hili:
 
Usikanyage kiongeza mwendo (Accelerator) hadi mwisho. Unapokanyaga kiongeza mwendo hadi mwisho unasababisha matumizi makubwa sana ya mafuta. Hivyo kupelekea upotevu wa mafuta usiokuwa na ulazima.
 
Hitimisho
Zilizojadiliwa hapa ni njia anuwai zitakazokuwezesha kuokoa mafuta unapoendesha gari. Ni dhahiri kuwa kupunguza matumizi ya mafuta ni jambo linalowezekana ikiwa utafanyia kazi hoja jadiliwa hapo juu, ikiwemo matengenezo ya gari kwa wakati pamoja na uendeshaji sahihi.
 
Back
Top Bottom