MAWASILIANO
Kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya watu wanaoshiriki/kufanya jambo pamoja ni kitu kibaya sana. Hivyo mara tu unapoona kwamba kuna jambo hulielewi au kunakitu kinakukera kiseme mapema ili kondoa kikwazo katika mawasiliano yenu. Kuna njia nyingi za kuweza kujadili tatizo na kulitatua lakini njia nzuri ni kuongea mkiwa pamoja (Uso kwa uso).
USIFANYE USICHOPENDA KUFANYIWA
Kila mara unapotaka kusema kitu, tafakari kama ni wewe ulikuwa unaambiwa maneno hayo na mtu mwingine ungejisikiaje. Hili litakusaidia kuepuka vitu ambavyo vitasababisha makwazo kwa rafiki zao na kufanya mahusiano yenye kuwa kwenye hatari.
TIMIZA WAJIBU WAKO
Kama timu kuna wakati mtahitajika kufanya kazi kila mtu mwenyewe ili kutimiza malengo yenu. Unapokuwa na jukumu la kufanya hakikisha unalifanya na unalifanya kwa usahihi. Mmoja wenu asipotimiza jukumu lake ataangusha timu nzima kitu ambacho wenzako hawatakifurahia.
MAZINGIRA
Mazingira manayofanyia kazi ni muhimu katika kuamua matokeo ya kazi yenu. Maeneo yanayozunguka eneo la kazi, Kelele, Mwanga, ufikaji wa eneo huweza kufanya kazi kuwa nzuri au mbaya. Siku zote kazi nzuri haiwezi kupatikana kama mazingira ni mabaya na kinyume ni kweli.
MAKOSA
Ni hakika kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, wote tunafanya makosa. Unapofanya kosa katika kazi lisiishie tu kuwa kosa bali jifunze kupitia kosa hilo ili uweze kuifanya kazi kwa usahihi wakati mwingine.
PONGEZI
Je! Umependa kitu mwenzako alichofanya, sema au kuandika? Kama ndiyo basi una kila sababu ya kumpongeza tena ukiwa na tabasamu la furaha. Pongezi huongeza morali na furaha katika kazi kwani mtu anaona kuwa jitihada zake zimeonekana. Hakuna mtu anayependa afanye kitu halafu kila mtu akipinge kuwa hakifai au aseme kimefanywa vibaya.
MATUSI/LUGHA MBAYA
Kuna vitu hupaswi kuvivumilia au kuvionea aibu na kuvuacha vipite kwani vitaharibu muhusiano wenu. Matusi, Kugombezwa/ kupigiwa kelele au kutolewa lugha ambayo siyo nzuri ni jambo ambalo hakuna anaelifurahia. Hivyo jambo kama hili likitokea na likakukwaza ni vyema mkalizungumza mapema.
UBISHI
Epuka sana ubishi usio na tija na pia kujifanya kwamba wewe ndio unafahamu zaidi ya washiriki wenzako na kwamba mawazo yako ndiyo yenye uhalali wa kusikilizwa. Hali hii itapelekea kupungua kwa ushirikiano kati yenu na hata ukiwa unakosea wenzako watakuacha kwa vile wewe ni mbishi, hushauriki. Hali ikishafikia hapa ni vigumu sana kuweza kufanikiwa.
Kuna faida ya wapenzi kuachana na kurudiana? Vipi kuhusu hasara zake? Hiyo ndiyo mada yetu ya leo kama inavyojieleza. Bila shaka unawajua watu ambao walikuwa wakiishi pamoja kimapenzi, iwe ni ndoa, uchumba au uhusiano wa kawaida ambao wamewahi kutengana na baadaye wakarudiana, iwe ni mara moja au zaidi.
Inawezekana hata wewe ukawa miongoni mwa watu wa aina hiyo, kwamba uliwahi kutengana na mtu umpendaye lakini baadaye ukajikuta unarudiana naye na kuanzisha upya uhusiano.
Je, kuna faida na madhara gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi unawachukuliaje?
Inawezekana kuwepo kwa aina hii ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya muda mkarudiana tena, na likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi za Kiafrika lakini hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano wa kimapenzi duniani kote.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanandoa au watu ambao wapo kwenye uhusiano imara wa kimapenzi, wamewahi kupitia kipindi hiki kigumu cha kutengana na kurudiana, wengine wakifanya hivyo mara kadhaa.
Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kutengana, hushindwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao hata kama bado wanapendana kwa kuona jamii itawashangaa kuwaona wakiwa pamoja tena baada ya kuachana kwa kashfa na vurugu kubwa.