Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso amejikuta akitiwa mbaroni na polisi mjini Bukoba kwa madai ya kumtwanga shabiki ngumi mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Kagera Sugar kupigwa 2-0 na Simba SC kwenye dimba la Kaitaba.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo (dressing-room) ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Kagera Sugar wakawa wanawarushia maneno makali (matusi) wachezaji hao.
 
Kufuatia maneno hayo, Nyoso alionekana kukosa uvumilivu na kuamua kumtwanga ngumi mmoja wa mashabiki hao ambaye alizimia papo hapo.
 
Mchungaji wa Kanisa la Bishop Mji wa Bwana lililopo Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es salaam amedai ametapeliwa nyumba na mchungaji mwenzake mkoani Morogoro. Mtumishi huyo wa Mungu aliyejitambulisha kwa jina la Jacob Jorum Swila alidai alimpangisha mchungaji huyo ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wake wa zamani na yeye kuamua kuiuza.
 
Baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo Januari 22, 2018, kumuhukumu, Salum Njete maarufu kama ‘Scorpion’ aliyekuwa akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho kwa adhabu ya kwenda jela miaka saba na kulipa fidia ya shilingi milioni 30 kwa kosa la kujeruhi na wizi, hatimaye muhusika aliyefanyiwa ukatili huo apingana na hukumu ya Mahakama kwa kudai amepewa adhabu ndogo.
 
Saidi Mrisho ambaye alifanyiwa tukio hilo la kinyama amefunguka na kusema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na kudai kuwa mtuhumiwa huyo ‘Scorpion’ alikuwa anastahili kufungwa maisha jela au na yeye angetobolewa macho kwa kuwa yeye sasa hivi anaishi maisha magumu yasiyoelezeka.
 
Hukumu hii imeniumiza sana, kwa sababu tayari ameshaniharibia maisha nina familia na nina watoto, Watoto wangu wanasoma sasa inabidi watoto wangu niwahamishie shule za serikali, kwa sababu sina pesa na maisha ninayoishi ni ya kupanga kwa sababu sina nyumba na nyumba niliyoahidiwa sikupewa.
 
Kwahiyo sasa mtu ambaye anakuharibia maisha, alikuwa anataka kupoteza malengo yangu, anafungwa miaka 7 na hiyo faini ya milioni 30. Kwa familia niliyonayo hiyo milioni 30 ni ndogo na hiyo hukumu ya miaka saba ni ndogo sana. Kwa hiyo inaniumiza sana na watoto wangu,“amesema Mrisho huku akibubujikwa na machozi ya hudhuni mapema baada ya Mahakama kutoa hukumu huku akieleza dhamira yake ya kutaka kuonana na RC Makonda na Rais Magufuli.
 
Kwa hili hapa mimi linaniumiza sana , nitaomba nitafika kwa Mkuu wa Mkoa, na nitaomba nifike kwa Mhe. Rais nampenda sana na anajitihada kubwa sana kwa Wananchi wake nitaomba anisaidie kwa hili,“amesema Mrisho.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, mnamo mwezi Septemba mwaka 2016 maeneo ya Buguruni Kwamnyamani, Said Mrisho akiwa maeneo hayo majira ya usiku alivamiwa, akaporwa vitu, akajeruhiwa tumboni na kutobolewa macho yake yote mawili tukio lililopelekea Mrisho kupatwa na upofu wa milele.
 
Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu klabu ya Liverpool kuondokewa na mshambuliaji wao Philippe Coutinho sasa pengo lingine huenda likawapata tena baada ya mchezaji wao mwingine, Daniel Sturridge kutangaza kuwa anataka kuondoka klabuni hapo.
 
Imeelezwa kuwa Sturridge anataka kuelekea Hispania kwa mkopo kunako klabu ya Sevilla ambapo Liverpool wanataka wamuuze kwa moja kwa moja kwa Euro milioni 30.
 
Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Uhispania limeandika kuwa klabu ya Sevilla ipo tayari kumlipa Sturridge mshahara wake wote kwa msimu huu.
 
Sturridge amekuwa akiugulia majeraha tangu Desemba 6, 2017 alipoumia wakati Liverpool ilipoiadhibu klabu ya Spartak Moscow goli 7-0 kwenye mchezo wa Klabu Bingwa barani Ulaya.
 
Back
Top Bottom