Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Amesema Nabii Tito alikamatwa na Polisi Januari 16, baada ya kuhojiwa alionekana kuwa na tatizo la akili na kuamua kumpeleka katika hospitali hiyo ya wagonjwa wa akili.
 
Amebainisha kuwa alipofanyiwa uchunguzi na daktari aliyemtaja kwa jina moja la Philipo alibaini kuwa nabii huyo ana tatizo hilo.

Nabii huyo amekuwa akionekana mitaani akihubiri huku akiwa anakunywa pombe.
 
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inaandaa utaratibu wa kisheria utakaowawezesha watu mashuhuri wanaotaka majina yao waitwe wanyamapori wa hifadhi hiyo, wakiwemo faru kulipia.
 
Akizungumza jana Januari 22, mwaka 2018 na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii waliotembelea hifadhi hiyo, mhifadhi mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Fredy Manongi amesema utaratibu huo utasaidia kuongeza mapato ya Ngorongoro.
 
Dk Manongi amesema wakati utaratibu huo ukifanyika hakuna majina mapya ambayo yatatolewa.

Awali Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) ,Joshua Nassari na Joseph Msukuma (Geita Mjini) waliotaka kujua mchakato wa wanyamapori kupewa majina ya viongozi.
 
Nassari amesema amepata taarifa kwamba kuna faru anaitwa Ndugai (Job-Spika wa Bunge), kutaka kujua sababu za kupewa jina hilo.

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo, Manongi amesema faru huyo kuitwa Ndugai kunatokana na Spika huyo wa Bunge kuwa mhifadhi, pia alikuwa mjumbe wa bodi ya Ngorongoro kwa muda mrefu.
 
Mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ilitoa habari njema za maendeleo ya teknolojia ya tiba kwamba kuanzia Machi mwaka huu itaanza kupandikiza figo.

Hospitali hiyo imesema wataalamu kwa ajili ya shughuli hiyo wapo na vifaa yaani mashine za kisasa kabisa kwa ajili ya upandikizaji figo nazo zinapatikana kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa kwa ufanisi.
 
Halafu uongozi umesema, ingawa upandikizaji wa figo katika hospitali hiyo utafanyika kwa mara ya kwanza, wamejipanga kuhakikisha unafanyika kwa mafanikio makubwa na kuandika historia kuwa hospitali ya pili baada ya Muhimbili.
 
Tunafahamu kwamba Hospitali ya Mkapa haitakuwa ya kwanza kupandikiza figo nchini bali kinachofurahisha katika hili ni kuwa sasa tiba ya magonjwa ambayo madaktari wake ama walikuwa wanapatikana nje ya nchi au Muhimbili tu sasa imeanza kusogezwa mikoani.
 
Tunafahamu kwamba Hospitali ya Mkapa haitakuwa ya kwanza kupandikiza figo nchini bali kinachofurahisha katika hili ni kuwa sasa tiba ya magonjwa ambayo madaktari wake ama walikuwa wanapatikana nje ya nchi au Muhimbili tu sasa imeanza kusogezwa mikoani.
 
26268804_338283663242124_768562171163443200_n.jpg

@halleberry @traceeellisross @lupitanyongo [HASHTAG]#sagawards[/HASHTAG]
 
Aidha tiba ya ugonjwa kama wa kansa kwa miaka mingi imekuwa ikilazimu wagonjwa kupelekwa Ocean Road pekee; magonjwa yanayohusiana na moyo wagonjwa wamekuwa wakipelekwa India hadi hivi karibuni ilipoanzishwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Muhimbili, na hivi karibuni Muhimbili imejengewa uwezo wa kuhudumia wenye matatizo ya usikivu.
 
Katika tiba ya moyo utaalamu umefikia hatua ya kuwawekea vifaa vya kusaidia mapigo ya moyo kwa watoto wengi ambao bila ya taasisi hiyo ama wangepoteza uhai au wangeigharimu Serikali mamilioni ya shilingi kuwapeleka nje ya nchi. Mafanikio haya hakika yanastahili pongezi maana ni juhudi za kuondokana na utegemezi.
 
Tunapongeza zaidi kwa sababu mara nyingi, kila Serikali inaposema inaboresha huduma zake huwa ni kuongeza uwezo wa Muhimbili na mara chache zinazoitwa hospitali za rufaa. Lakini sasa Serikali imevunja mwiko huo imepeleka huduma hii muhimu na ghali kwa Hospitali ya Mkapa tena katikati ya nchi.
 
Upandikizaji wa figo ni teknolojia ngeni ndiyo maana katika Hospitali ya Mkapa utafanywa na madaktari wa Tanzania kwa kushirikiana na wenzao kutoka Japan kwa kuwa wameanza siku nyingi.
 
Ushirikiano huu ni wa kawaida katika siku za mwanzo na kutokana na ukweli kuwa kumsomesha daktari hadi afikie kubobea katika fani yoyote kama hizo za figo na moyo ni gharama na inachukua muda, lakini mkazo uwe kupata wa kwetu kwani hiyo ndiyo njia pekee ambayo itawezesha nchi kupata madaktari wake tena wa kutosha.
 
Vilevile, Hospitali ya Mkapa imesema kwa kuanzia ina wagonjwa wawili watakaopandikizwa figo na kwamba gharama zao zitalipwa na chuo na hospitali kwa sababu mpaka sasa gharama halisi ya kufanya upandikizaji haijapangwa.

Tunatoa rai, wakati utakapofika, wizara ya afya ipange gharama nafuu ili watu wengi wenye uhitaji waweze kumudu na kuokoa maisha yao.
 
Back
Top Bottom