Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

AINA:
Kuna aina nyingi za pilipili hoho. Baadhi ya aina zinazostawishwa nchini ni California, Wonder, Emerald Giant, Sweet Neapotitan, Yolo Wonder, Pimiento na Keystone Resistant Giant. Aina zingine ni kama vile Ruby King, Ruby Giant, Libert Bell na Yolo Wonder B.
 
KUPANDA MBEGU:
Mbegu zinaweza kupandwa moja kwa moja shambani au kuoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye kuhamishiwa shambani.
 
Kuotesha mbegu Kitaluni.
Kabla ya kusia mbegu tengeneza tuta lenye upana wa mita moja. Urefu wa tuta utategemea eneo la shamba linalotarajiwa kupandwa. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo mbili au zaidi katika eneo la mita mraba moja.
 
Changanya mbolea na udongo vizuri, kisha tengeneza vifereji vyenye nafasi ya sentimeta 10 hadi 15 kutoka kifereji hadi kingine. Kina cha kifereji kiwe sentimeta moja hadi tatu katika eneo hilo, kiasi hiki kitatoa miche ambayo itatosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100.
 
Baada ya kusia fukia kwa kutumia udongo laini au mbolea za asili zilizooza vizuri. Weka matandazo na kisha mwagilia maji. Endelea kumwagilia kitalu kila siku asubuhi na jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku sita hadi 10. Mara zitakapoota ondoa matandazo. Endelea kumwagilia maji hadi wakati miche inakuwa tayari kwa kupandikizwa
 
KUTAYARISHA SHAMBA
Tayarisha shamba vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche, katua ardhi katika kina cha kutosha sentimeta 30 kwenda chini, weka mbolea za asili kiasi cha tani 10 hadi 15 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na debe moja kwa eneo la mita mraba moja changanya mbolea na udongo vizuri.
 
Ikiwa eneo hilo lina upungufu wa madini aina ya fosiforasi kama itakavyothibitishwa na wataalam, weka mbolea ya chokaa aina ya TSP. Kiasi kinachotakiwa ni kilo 200 kwa hekta. Lainisha udongo siku tatu au tano kabla ya kupandikiza miche.
 
KUPANDIKIZA MICHE:
Miche huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki nne hadi 10. Wakati huu huwa na majani sita hadi manane na urefu wa sentimeta 10 hadi 15.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…