Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

-20664982801438443236.jpg
 
Kuwapa wafanyakazi wako wanaojituma kazi nyingi sana inawafanya waone wanaadhibiwa kwa tabia yao ya kujituma. Kama ni lazima uongeze kazi kwa wafanyakazi wako wenye uwezo, ni bora ukawaongezea hadhi zaidi pia. Ongezeko la mshahara na cheo huwa inafanya kazi unazoziongeza zikubalike kirahisi zaidi.
 
Kama utakuwa unawaongezea kazi kwa sababu wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi, bila kubadilisha lolote, wengi watajikuta wanatafuta kazi sehemu nyingine ambapo wanaweza kupata wanachotaka.
 
Kutothamini mchango na kazi kubwa inayofanywa
Ni rahisi sana kudharau jambo kama kumpa hongera mfanyakazi kwa kumgusa mgongoni inaweza kuwa na maana kubwa kiasi gani kwa mfanyakazi wako, hasa kwa wale wenye utendaji wa juu ambao huwa wanajituma wenyewe bila kusukumwa.
 
Kutojali wafanyakazi
Zaidi ya nusu ya wafanyakazi wanaoacha ajira zao wanafanya hivyo kwa sababu ya uhusiano kati yao na bosi. Makampuni yenye mafanikio zaidi yanahakikisha kuwa mabosi wanaoendesha kampuni hizo wana uwezo mkubwa wa kuhakikisha wafanyakazi wanafata taaluma lakini pia kuweka utu mbele kwenye uhusiano na wafanyakazi hao.
 
Kuna baadhi ya mabosi wanafurahia mafanikio ya wafanyakazi wao, kufariji walio kwenye matatizo, kuwapa changamoto na kuwaambia ukweli wafanyakazi wao, hata kama itawaumiza. Mabosi ambao hawajali maisha ya wafanyakazi wao watakimbiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Kuna baadhi ya mabosi wanafurahia mafanikio ya wafanyakazi wao, kufariji walio kwenye matatizo, kuwapa changamoto na kuwaambia ukweli wafanyakazi wao, hata kama itawaumiza. Mabosi ambao hawajali maisha ya wafanyakazi wao watakimbiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Kutotimiza ahadi anazotoa
Unapotoa ahadi kwa watu inakuweka kwenye nafasi ya kuwafurahisha sana au kusababisha waondoke kabisa. Unapotimiza ahadi zako, wafanyakazi wako wanakuongezea heshima zaidi kwa sababu unawathibitishia kwamba unastahili kuaminiwa na unatimiza kila unaloahidi (vigezo viwili vikubwa sana kwa kila bosi kuwa navyo). Lakini unapokuwa hutimizi ahadi zako ni rahisi kuonekana hujali, una dharau na huwaheshimu wafanyakazi wako.
 
Back
Top Bottom