Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maambukizi katika mirija ni matokeo ya kusambaa kwa maambukizi haya toka ukeni, katika kuta za kizazi hadi kwenye mirija na vifuko vya mayai.
Maambukizi yakiwa makali na ya muda mrefu husambaa nje ya kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Pelvic Perisoneum.
 
Maambukizi katika mirija ya uzazi yapo katika makundi mawili, kwanza Acute ni yale sugu ‘Chronic Salpingitis’ na pili ni yale makali ‘Chronic Salpingitis’, maambukizi haya hutokea kwa vipindi tofauti kutokana na ukali wa ugonjwa.
Dalili za ugonjwa
 
Athari za tatizo
Maambukizi yanaweza kusambaa hadi katika mirija toka ukeni hadi ndani ya kizazi pale mwanamke anapokuwa katika damu ya hedhi na kama damu itarudi kwa juu, hii siyo hali ya kawaida na tutakuja kuiona katika makala zijazo.
 
Magonjwa yaenezwayo kwa ngono pia ni tatizo kubwa katika uharibifu wa mirija.
Bakteria wanaosababisha tatizo hili la maambukizi na uharibifu wa mirija ni ‘Neisseria Gonorrhea’ ambayo husababisha ugonjwa wa kisonono au gono.
 
Wanawake wengi huwa hawapati dalili za awali za ugonjwa, dalili zinapojitokeza tatizo hili huchangia wanawake wengi kutafuta tiba kwa muda mrefu na wengi hukusanyika katika kliniki za magonjwa ya kinamama.
 
Back
Top Bottom