Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jitahidi ubadilike na fahamu kwamba kufanya hivyo kukiendelea sana kwako itakuwa tena sio mazoea bali ni tabia na siku zote mazoea hujenga tabia, utajikuta huachi hata kama utampata wa kukutimizia haja zako (Mke) kwani hutoridhika naye kwa athari ya mkono wako.
 
Fahamu pia kuwa kutafuta msichana (Girlfriend) sio njia sahihi kwani ndiyo sababu ya kuharibu jamii kwa kuwaharibia maisha yao kwa kuwapa ujauzito wakiwa mashuleni, kusambaza maradhi na kuleta watoto wa mitaani (Street Children).
 
Watu wengi wamekuwa wavivu wa kunywa maji, hawajui kuwa maji ni muhimu sana katika mwili na yanahitajika kwa kiwango kikubwa. Wengi hawajui kuwa maji ni tiba ya maradhi mengi. Ili maji yawe tiba ya magonjwa, ni lazima ufuate kanuni ya namna ya kuyatumia.
 
Maji husafisha figo. Figo kuwa na uchafu ama vimawe vidogo vidogo husababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Maji huyeyusha takataka zote zonazojiunda kutengeneza vijimawe katika mkojo. Hivyo kunywa maji mengi kutasaidia kusafisha figo zako.
 
Kunywa maji punde tu unapoamka. Mwili wako hupoteza kiwango kikubwa cha maji unapokuwa umelala, hivyo jitahidi kunywa maji kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. Unapokunywa maji asubuhi, husaidia kuondoa sumu zote zilizotengenezwa mwilini ulipokuwa umelala.
 
Jitahidi kunywa glass 8 mpaka 12 kwa siku. Kulingana na kliniki ya afya ya Mayo, mtu mwenye uzito wa kilo 55 anatakiwa kunywa maji glass 8 wakati mtu mwenye uzito wa kilo 87 anatakiwa kunywa maji glass 12 kwa siku. Inabidi kuhakikisha kuwa rangi ya mkojo inakuwa nyepesi. Unashauriwa kutokunywa zaidi ya glass 16 kwa siku.
 
Usisubiri mpaka kiu ikupate ndipo unyewe maji. Wakati unapohisi kiu, inawezekana umeshapunguza glass 2 katika kiwango cha maji kinachotakiwa mwilini. Wazee huwa hawapatwi na kiu mara kwa mara, kwahiyo wanahitajika kunywa maji hata pasipo kuhisi kiu.
 
Kunywa maji mengi kama hali ya hewa ni ya joto. Watu wanaoishi katika maeneo yenye joto kama Dar es salaam, wanatakiwa kunywa maji kwa wingi. Watu hawa wako katika hatari ya kupata matatizo ya figo kama hawatakunywa maji kwa wingi ukilinganisga na watu wanaoishi katika maeneo yenye baridi kama vile Iringa na Mbeya.
 
Kunywa maji, na siyo vinywaji baridi, vileo ama kahawa. Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa chai, soda na kahawa vinaweza kuongeza kiwango cha maji mwilini. Ingawa vinywaji hivyo vina kiwango kikubwa cha kaboni na sukari ambayo inaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari na mifupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…