Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ecdcd5343aeeac6418fba42c35db5ba5.jpg
 
Nimeipenda sana hii. Na dakika chache zilizopita kabla sijaiona hii nilikuwa naongea mtu na kumwambia mshangao wangu mkubwa wa udikteta uchwara unaofanywa na FP wa Marekani na chama chake cha Republicans.
Kuna mchambuzi mmoja nilikuwa namsikiliza hapa amenifikirisha sana. Anasema kwamba kama Marekani ambaye kimsingi ndiye alikuwa mtetezi na mlinzi mkuu wa demokrasia duniani kote leo hii naye ana kiongozi anayekoromea vyombo huru vya habari, mahakama na hataki kabisa kusikia maoni kinzani, mustakabali wa demokrasia kama mfumo duniani ukoje? Anadai kwamba kuinukia kwa madikteta-vuguvugu (au populist/ nationalists kama alivyowaita yeye) wasiojali misingi ya kidemokrasia karibu duniani kote kuna maana gani? Anadodosa kwamba inawezekana pengine demokrasia kama mfumo wa kijumla umechakaa na dunia ama inajaribu kutafuta mfumo mwingine au kila nchi inajaribu kuunda "demokrasia" yake kulingana na matakwa yake, utamaduni wake, historia yake na uchumi wake. Wewe kama mchambuzi na GT unaonaje kuhusu maoni kama haya?
 
Back
Top Bottom