Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hebu fikiria umepanda daladala, halafu kondakta anaitisha nauli. Ukiangalia mfukoni una shilingi mia mbili tu, pesa nyingine yote umeisahau nyumbani. Ni hali gani huwa inakupata?
 
Kama huwa unapata wakati mgumu kwa jambo hilo dogo tu, je inakuwaje pale ambapo unataka kuwaomba watu wakuchangie mamilioni kwa ajili ya kuifanikisha harusi yako ambayo kwao haina faida yoyote?
 
Usipange bajeti ambayo hutoweza kuimudu
Harusi nyingi hufanywa kwa gharama kubwa sana. Watu wengi wanaofunga ndoa hupenda kupanga bajeti kubwa ambayo wengine hata hawawezi kuzifikia.
 
Vile vile usipange bajeti ambayo itakuwa ngumu kufikiwa na kamati yako ya harusi
Unapopanga bajeti ya harusi yako, hakikisha kuwa haitokuwa mzigo kwa wale unaowalenga kukuchangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…