Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya leo Jumanne, baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.
Muhtasari
Raila Odinga anadai alishinda uchaguzi urais wa tarehe 8 Agosti 2017
Mahakama ya Juu ilibatilisha matokeo ya uchaguzi huo wa Agosti na kuagiza uchaguzi urudiwe, lakini Bw Odinga akasusia
Odinga amesema hatambui ushindi wa Bw Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio wa 26 Oktoba
Serikali imeonya kuwa hatua ya kuapishwa kwa Bw Odinga ni uhaini wa kiwango cha juu