Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b624d1eb4c4ae3b50fa58dc3fa50fd09.jpg
 
“Ni kweli tutaanza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole kwa sababu hiyo ndiyo njia salama ya usajili,” alisema.
 
Alisema katika mpango huo wa majaribio wataanza kusajili katika mikoa minne ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, utafanyika Zanzibar. “Katika mikoa hiyo tutaanza kusajili wateja wapya kwa kutumia alama za vidole,” alisema.
 
Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesitisha kuwaondoa wananchi waliopo hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Kimara.

Awamu hiyo ya pili ya kazi ya kuwaondoa wananchi katika barabara hiyo, imesitishwa kupisha mradi wa Benki ya Dunia (WB) wa kuboresha miundombinu ya BRT awamu ya kwanza kati ya Kibo na Kimara.

Takriban nyumba 1,200 zilizopo ndani ya mita 90 kutoka Ubungo hadi Kimara zinatakiwa kubomolewa kupisha upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi sita.
 
Akizungumza jana meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama alisema wananchi wa eneo hilo wamefahamishwa kuhusu usitishwaji huo kupitia viongozi wa serikali za mtaa.

Ndyamukama alisema nyumba hizo hazitabomolewa hadi mradi wa BRT utakapokamilika.

“Ujenzi umeanza, mkandarasi anaendelea na kazi. Tunatarajia ndani ya mwaka mmoja utakuwa umekamilika,” alisema Ndyamukama na kuongeza: “Kuhusu idadi ya nyumba ambazo zilitakiwa kuondolewa sina takwimu sahihi, ila kwa nyumba za Ubungo hadi Kona tulishaweka alama ya X.”
 
Kimara hadi Kiluvya

Wakati upanuzi wa barabara kutoka Kimara hadi Kiluvya ukitarajiwa kuanza, nyumba 1,183 zikiwamo shule na za ibada zimebomolewa.

Ndymukama alisema kampuni ya ujenzi ya Estim Construction Ltd, imepewa zabuni ya mradi wa upanuzi wa barabara hiyo baada ya kukidhi vigezo.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa njia za juu katika makutano ya Ubungo, katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Joseph Nyamhanga alisema Sh33 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuanza upanuzi wa barabara ya Morogoro.
 
Alisema kwa sasa barabara hiyo itapanuliwa kutoka njia mbili na kuwa sita na kwamba, mradi huo unagharamiwa na Serikali lengo ni kupunguza msongamano.

Katika hatua nyingine, Serikali imeagiza mamlaka zinazohusika na ubomoaji wa jengo la Tanesco kukamilisha ifikapo Februari Mosi.

Mkurugenzi mtendaji uwezeshaji wa Tanesco, Khalid James alisema kuchelewa kubomolewa jengo hilo kumetokana na ukosefu wa vifaa maalumu vya kubomolea.
 
Back
Top Bottom