Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mabasi ya wafuasi wa upinzani yazuiwa Voi
Mabasi matatu yaliyokuwa yanawasafirisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaelekea Nairobi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga yamekamatwa na maafisa wa polisi katika mji wa Voi, katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Nairobi.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole
 
Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka hiyo, Semu Mwakyanjala alisema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.
 
Mwakyanjala alitoa ufafanuzi huo baada ya mwandishi wa Mwananchi kuuliza kuhusu ujumbe unaotumwa kwa wateja kutoka kampuni za simu za mkononi ukiwajulisha kuhusu usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.
 
Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,” ni ujumbe ambao umekuwa ukitumwa kwa wateja wa kampuni za simu.
 
Mwakyanjala alisema mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.
 
Mwakyanjala alisema mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.
 
Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…