Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

e2cc08ade6cd4a1fd5dd32d540f0fbb6.jpg
[emoji56] [emoji56]
 
Wawili hao wametofautiana ndani ya bunge baada ya mbunge Bakari kuhoji kuhusu ubovu wa mashine hizo uwanja wa ndege wa Pemba ambayo ni mbovu na haifanyi kazi inayotakiwa jambo linalosababisha kupitishwa kwa mizigo isiyokuwa rasmi.

Mbunge huyo amelalamikia mashine hiyo kwamba imekuwa ni kero kwa wasafiri na uchochoro wa kupitishia dawa za kulevya zinazoingia au kutoka.
 
Hata hivyo, Naibu Waziri Nditiye akasimama na kupinga kauli hiyo akisema mashine hiyo inafanya kazi kama ilivyo mashine nyingine na wamekuwa wakifuatilia utendaji kazi wake hatua kwa hatua.

“Wakati wote tumekuwa na mawasiliano na wenzetu wa Pemba kuhusu mashine hiyo, ukweli ni nzima na inafanya kazi masaa yote na hakuna shida yoyote katika eneo hilo,” amesema Nditiye.
 
Kauli yake ilimfanya Bakari kuwasha kipaza sauti na kuanza kupiga kelele kuwa mashine hiyo ni mbovu na kuwa Naibu Waziri alikuwa analidanganya bunge hivyo akataka kutoa maelezo.

Naibu Spika Dk Tulia Akson alimuinua Waziri Jenister Mhagama kwa ajili ya kutuliza malumbano hayo akisema Serikali imepokea taarifa hizo na kuahidi kuzifuatilia ili kama kuna upungufu uweze kurekebishwa.
 
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Kiembe Samaki Ibrahimu Mohamed Raza (CCM) ametaka kujua ni lini serikali itachukua hatua kwa kuwasaidia vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Anton Mavunde amekiri kuwa Serikali inatambua tatizo la matumizi ya dawa za kulevya na athari zake kubwa kwanguvu kubwa ya vijana.
 
Mavunde amesema mapambano ya dawa hizo yanaendelea ambapo katika kipindi cha mwaka jana wamefanikiwa kukamata kilo 196 za dawa aina ya heroin tani 47 za bangi na tani 7 za mirungi.

Wakati huohuo Mavunde amesema Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha kituo kikubwa cha kuwapatia waathirika tiba kwa njia ya kazi (occupational therapy) ambapo mafunzo ya stadi za kazi mbalimbali yatatolewa na kituo hicho kitajengwa eneo la Itega mkoani Dodoma.
 
Serikali imesema hakuna vikwazo katika uhamisho wa walimu na kutaka jambo hilo lifanywe na wahusika kwa kufuata taratibu.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 30, 2018 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Rehema Juma Migilli.
 
sababu mbalimbali.

Pia, amehoji lini Serikali itatoa mafunzo kwa walimu wanaotolewa shule za sekondari na kupelekwa shule za msingi ili waweze kuendana na mitaala inayofundishwa huko.

Katika majibu yake, Kakunda amesema walimu wanaozingatia taratibu zote na kanuni za utumishi huweza kuhamishwa bila shida.
 
Mfano, katika kipindi cha Julai 2017 hadi Januari 2018, walimu 2,755 kwa nchi nzima walihamishwa na wengine taratibu zinaendelea,” amesema.

Kuhusu kuwapa mafunzo walimu wanaohamishwa kutoka sekondari kwenda msingi, amesema hawawezi kupewa mafunzo kwa sababu wengi walipandishwa kutoka msingi kwenda sekondari.
 
Back
Top Bottom