carbamazepine
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 46,577
- 285,648
Nadhani miaka michache iliyopita walikubali kuilipa fidia serikali ya Namibia. Wakenya nao wakaikomalia serikali ya Uingereza ikawalipa kwa masaibu ya Mau Mau. Wajerumani tungewakomalia pengine nasi wangetulipa kwa ukatili wao wa vita vya Majimaji; na masaibu mengineyo.1. WAJERUMANI WALIVYOSAFISHA KABILA LA WAHERERO.
Baada ya kusikia fununu ya madini Namibia, Wajerumani walikuja na kutawala pwani ya nchi hiyo na kukaa katikati ya kabila la waherero. Kosa kubwa wenyeji walipojifanya wabishi. Walizungukwa pande zote, Upande uliobaki ulikuwa ni jangwa ambalo visima vyote vya maji mjerumani alivitia sumu. Ukimbie unywe maji ya sumu au ufe na kiu jangwani au ukutane na risasi. Asilimia 80 ya wenyeji wote waliuwawa kikatili sana bila huruma.
Wakenya bhanaRaila anaapa....
Mpaka anakufa Chinua Achebe (Muigbo) alikuwa akilalamikia ukatili waliofanyiwa watu wake katika vita hivyo...9: VITA VYA BIAFRA - NIGERIA.
Tofauti na tanzania tuna makabila mengi yanayopendana, na Nyerere alisaidia kikubwa, Hii haikuwa hivyo Nigeria. Wanamakabila zaidi ya 300 na yalikuwa karibu karibu kilichosababisha ugomvi mara kwa mara.Tatizo lilianza pale Kabila/kundi kubwa la IGBO walipojikatia nchi na kutengeneza nchi yao ya BIAFRA eneo tajiri kwa mafuta. Serikali haraka ikataka kuwarudisha. Kwa mbinu katili kabisa hata kuzuia chakula na maji yasielekee BIAFRA. Inasemekana kila siku walikuwa wanakufa watu zaidi ya 5000 wengi wao IGBO. Watu zaidi ya Milioni 3 walikufa hadi vita kuisha.