Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Juma lililopita, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema kwamba anataka wahamiaji wanaoingia Marekani wawe wametoka nchini Norway badala ya nchi za Afrika alizoziita tundu la choo (shithole). Katika mkutano wa kiuchumi unaoendelea nchini Uswisi, Trump ataweza kujionea kwanini wahamiaji wanaoingia Marekani hawawezi kutokea Norway.
 
Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Dunia (WEF), Norway ndiyo nchi bora zaidi kwa binadamu kuishi duniani. Wachunguzi kutoka katika jukwaa hilo wametoa tuzo hiyo kwa Norway baada ya kufanya uchunguzi ambao haukuhusisha tu ukuaji wa uchumi (pato la taifa), lakini pia hali ya maisha ya wananchi.
 
Wachunguzi hao walilazimika kupiga hatua ya ziada na kuangalia maisha ya wananchi kwa sababu, unaweza ukawa na uchumi unaokuwa vizuri na uwepo wa viwanda, lakini maisha ya wananchi yakawa yanaathirika kwa kiasi kikubwa na shughuli hizo mfano uchafu kutoka kwenye viwanda na kufanya wananchi waugue.
 
Wafanyabiashara kwa upande wao wanaamini kwamba, kukua kwa uchumi ndio kipimo bora zaidi cha kupima ubora wa maisha ya wananchi, kwa sababu ukuaji huo unamgusa kila mwananchi. Lakini wachambuzi hao walipinga kauli hiyo na kutolea mfano Marekani ambayo uchumi wake umekuwa ukikua lakini kuna tabaka la watu bado wamo katika umasikini.
 
Katika mkutano wa uchumi unaoendelea Davos nchini Uswisi, WEF wamewatahadharisha wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa kutokuamini kwamba ukuaji wa uchumi ndio suluhusho la matatizo ya kijamii.
 
WEF imetoa wito kwa nchi mbalimbali kuangalia vitu vingine kama kipato cha mtu binafsi, utofauti wa walionacho na wasionacho katika jamii, ujumuishi wa wananchi, ukuaji na maendeleo, uchafuzi wa mazingira, madeni, umasikini, pale wanapotaka kupima kama nchi imeendelea ama la.
 
Utafiti uliofanywa na Wanasayansi kutoka National Research Council umegundua kuwa ulaji wa chipsi au viazi vilivyokaangwa mara mbili au zaidi kwa wiki husababisha vifo vya mapema kwa vijana kwa zaidi ya 70%.
 
Akielezea utafiti huo Dr. Nicola Veronese amesema ulaji wa viazi hauleti tatizo lolote la kiafya bali vinapokaangwa ndipo hupelekea kiwango kikubwa cha kolestro kunyonywa na mishipa ya damu pindi mtu anapokula hivyo kusababisha ugonjwa wa cardiovascular.
 
Katika utafiti huu watu 4,440 walihusishwa na walikula chipsi mara tatu kwa wiki kwa muda wa miaka minane ambapo zaidi ya watu 236 walifariki kutokana na ugonjwa wa cardiovascular kuliko magonjwa mengine.
 
920f3976b24baeab99b67329d595f56a.jpg
Mtambo wa nguvu hahahaaa
 
Back
Top Bottom