Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Madeni
Hakuna jambo linalowakosesha baadhi ya watu amani kama madeni. Wapo waliofikia hatua ya kujiua kwa sababu ya kudaiwa kila kona. Licha ya kwamba kila mmoja kuna wakati anakopa, hutakiwi kuiendekeza tabia hii na kama unaweza, epuka kukopa na utajiona ni mtu huru.
 
Kukosa chanzo cha kipato
Maisha ya sasa bila kufanya kazi huwezi kuwa na maisha mazuri kwani ndiyo inayoweza kukupatia kipato cha kuyaendesha maisha yako. Hata hivyo, ili kukufanya uweze kujikimu kimaisha, hakikisha unafanya kazi bila kuchagua kazi.
 
Ugumu wa maisha
Binadamu yeyote lazima apate mahitaji muhimu kama vile chakula, mavazi, sehemu nzuri ya kulala na matibabu akiumwa. Endapo utajihakikishia yote hayo katika kiwango kinachostahili, maisha yako yatakuwa ya furaha.
 
Kuishiwa
Fedha ndo’ ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya binadamu, ukikosa fedha lazima kichwa kikuume. Wapo ambao wanakosa amani wanapofikiria matatizo yanayoweza kuwakumba huku wakiwa hawana pesa kabisa.
 
27355960_2400349130205069_62051326185344214_o.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kukosa upendo/Kuchukiwa
Hata uwe na mamilioni vipi, kama watu wanaokuzunguka hawakupendi, huwezi kuwa na furaha. Ndiyo maana unatakiwa kutumia gharama yoyote kujihakikisha upendo kutoka kwa ndugu zako, majirani, marafiki na watu ambao unakutana nao katika mihangaiko yako.
 
Mkusanyiko wa matatizo
Hakuna binadamu asiyekumbwa na matatizo ambayo mara nyingi hufanya amani itoweke. Hata hivyo, inaelezwa kuwa, ili kuepuka msongo wa mawazo, hakikisha kila tatizo linalotokea mbele yako unalitatua haraka.
 
Back
Top Bottom