mfano mzuri ni pale wewe baba unapotoa ahadi kwa wanao ya kuwa wakifaulu vizuri darasani utawanunulia zawadi, lakini baada ya kutambua kuwa wamefaulu ukasema tena hutoi zawadi uliyoahidi,
huo ni sawa na uongo kwa sababu umeshindwa kutimiza ahadi yako, hii moja kwa moja inakuwa imepunguzia imani kwa watoto wako ya kukuamini kwa kile uanchokisema hata kama hawatakwambia.
Katika biashara
Hapa sasa kuna changamoto kubwa itokanayo na kusimamia kwenye ukweli, mfano utakuta mtu anauza bidhaa ambazo anajua kabisa ni feki, lakini hataki kumweka wazi mteja wake kwa sababu anahofia ya kuwa pengine ataacha kununua hiyo bidhaa kwa kumwambia ukweli.
lakini furaha hiyo ni ya muda tu, usitarajie mteja huyo kama atarudi tena kununua bidhaa hiyo kwako hata kama utaleta bidhaa halisi(yaani original) siku nyingine.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.