Najua utashangaa lakini ukweli ni kwamba wengi ambao wanakuwa na matatizo huwa hawajui tatizo hasa walilonalo ni nini. Na hivyo wanapokazana kulitatua wanashindwa, kwa sababu kama hujajua kiini cha tatizo huwezi kulitatua.
Mara nyingi watu wamekuwa wakiangalia madhara ya tatizo, badala ya kuangalia chanzo kikuu cha tatizo. Huwezi kutibu tatizo kwa kutibu madhara, badala yake unahitaji kuzama ndani na kujua chanzo hasa cha tatizo ni nini.
jiulize tena kwa nini wateja ni wachache, hapo utapata majibu mengine, kwa kila jibu jiulize tena kwa nini? Mpaka utafika mahali na kuona hiki ndio kiini kikuu cha tatizo.
Hatua ya pili; orodhesha hatua unazoweza kuchukua.
Baada ya kujua nini hasa ndiyo tatizo, sasa anza kuorodhesha kila hatua unayoweza kuchukua. Andika kila suluhisho linalowezekana kwenye tatizo ulilonalo.
Hakikisha unakuwa muwazi na unaandika kila wazo linalokuja kwenye kichwa chako, hata kama litaonekana ni la hovyo au haliwezekani, wewe orodhesha. Ni kwa njia hii ndiyo unaweza kupata njia bora kabisa za kukabiliana na tatizo unalokutana nalo.
Hatua ya tatu; andika faida na hasara za kila suluhisho.
Baada ya kuorodhesha hatua zote unazoweza kuchukua, yaani kila aina ya suluhisho unaloweza kuchukua, sasa unakwenda kuchambua suluhisho moja baada ya jingine.
Andika kila suluhisho na gawa pande mbili, upande mmoja andika faida utakayopata kama utachukua hatua hiyo, na upande wa pili andika hasara za kuchukua hatua hiyo.
Baada ya kujua faida na hasara za kila suluhisho, sasa unaweza kuchagua suluhisho sahihi kwako kufanyia kazi. Hapa angalia lile ambalo lina faida kubwa na nzuri na hasara kidogo.
Chagua suluhisho ambalo una uhakika unaweza kulifanya na hutokuja kujutia hapo baadaye. Pia hakikisha unaweza kusimamia suluhisho hilo bila ya kutetereka na kuweza kulitetea kwa wengine.
Chagua suluhisho ambalo una uhakika unaweza kulifanya na hutokuja kujutia hapo baadaye. Pia hakikisha unaweza kusimamia suluhisho hilo bila ya kutetereka na kuweza kulitetea kwa wengine.
Hatua ya tano; fanya mapitio ya suluhisho ulilochukua.
Ukishachukua hatua siyo mwisho, bali unahitaji kuwa unafanya mapitio na tathmini ya ile hatua uliyochagua kuchukua. Je inaleta matokeo ambayo ulitarajia kupata? Je kuna changamoto nyingine zinaibuka?
Bila ya kufanya tathmini unaweza kushangaa muda unakwenda lakini tatizo linaendelea kuwepo licha ya kupata suluhisho. Unapofanya tathmini unaona ni wapi panahitaji mkazo zaidi na wapi pako vizuri.
Hizo ndizo hatua tano muhimu za kufuata pale unapotaka kutatua tatizo lolote unalokutana nalo. Fuata hatua zote tano kwa mfuatano, usikimbilie hatua ya juu kama ya chini bado hujaikamilisha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.