Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anayetuhumiwa kumuua ‘Radio’ akamatwa : Polisi wa Mji wa Katwe Uganda, wamemkamata kijana Godfrey Wamala ambaye ametajwa kuhusika na shambulio la mwili lilopelekea kifo cha msanii Mowzey Radio. . Wamala mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa katika eneo la Kyengera alipokuwa amejificha kwa siku kadhaa nyumbani kwa rafiki yake. Wamala amehamishiwa mjini Entebbe ambapo Polisi wamesema watamfungulia mashtaka ya mauaji.
 
Kijana Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.

Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.

Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.
 
Si ajabu wajanja wanakafurumua saa hizi [emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️
D: D: D
 
8152e8bf2ad3c94a9ac4f7c782f79920.jpg
 
Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Kiongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya kujiapisha kuwa Rais wa watu wa nchini hiyo, Hatimaye Rais wa Kenya anayetambulika kikatiba Uhuru Kenyatta amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo.
 
Rais Kenyatta amesema kuwa kujenga taifa ni kazi kubwa lakini kubomoa ni muda mfupi hivyo amemshauri Raila Odinga kuacha maneno yenye mizozo na kuchafuana nje ya nchi kwani kushindwa kwenye uchaguzi ni jambo la kawaida hata yeye alishawahi kushindwa na akajipanga tena.
 
Kujenga ni ngumu lakini kupasua ni dakika moja, lakini hawaoni tabu kupasua afadhali apasue apate uongozi, awe mkubwa, ukubwa sio kiti ukubwa ukubwa ni vitendo ambavyo unawatendea wananchi ambao unataka kuwaongoza, na hivyo hivyo hata sisi tumekuwa twahimiza ni nini unawatendea wananchi wako. ukiwa umetoka nchi yako unaenda kutembea nchi nyingine kusema wale wanaoongoza kule wanastahili kufungwa. Si uje hapa Kenya kwetu utuambie,“amesema Uhuru Kenyatta huku akimshauri jambo la kufanya Raila Odinga.
 
Huwezi kufanikiwa kwa kumtakia mwenzio mabaya, omba mwenyezi Mungu na uombe wananchi kwa njia tulivu uoneshe sera zako tofauti na sera za wale wengine na wananchi sio wajinga wapo na ujuzi wakuamua ni nani wanataka na nani hawataki. Kama hawakutaki safari hii we pumzika wacha wale wengine waendelee, mimi nimegombea mara nyingi,
 
mimi nimewahi kusimama hii kiti nikashindwa na nikakaa nikatulia, Nikasema eehh Mwenyezi Mungu basi hii sio nafasi yangu wakati hii na nikakubali kushindwa, sasa ninaongoza na nitaongoza mpaka wananchi waseme basi wewe tulia, sasa shida iko wapi na tunabaki tunachafuana hapa kila siku, Lets us work together, Lets us keep Kenya moving ahead, lets us provide services to our people mambo hayo ndiyo ya muhimu na ndivyo tutaendelea na waseme na waseme hawatutishi,“amesema Rais Kenyatta
 
Back
Top Bottom