2 . Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huleta madhara katika mwili wa binadamu mara nyingi sana, mfano kuumwa kichwa, kuongezeka uzito, kuota vipele na hata vidonda vya tumbo, na kama nilivyosema awali , kama tayari umeshajua kwamba hedhi imechelewa msongo wa mawazo unaoupata kwa kufikiri sababu ni mimba ikiwa haukuwa umeitarajia unaweza kufanya mwili usiwe katika hali yake ya kawaida tena na hivyo kuendelea kusababisha kuchelewa kwa siku za hedhi zaidi na zaidi. Kwenye mwili wa mwanadamu kuna homoni mbili ziitwazo ‘adrenaline na cortisol’.
Hizi hufanya maamuzi kwenye mwili ya kipi kinaumuhimu zaidi ya kingine mpaka msongo wa mawazo utakapokuisha. Mara nyingi homini hizi huamua kuanza kazi katika vitu kama msukumo wa damu na gesi mapafuni, huku kazi nyingine kama mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kizazi kufuatia baadae na hivyo hata hedhi itachelewa kushuka kama tatizo ndio hilo.